Bahati asema sababu ya kuwazuia marafiki wa Diana kuhudhuria Ruracio yake

Afafanua kuwa kulingana na tamaduni,wazazi wa bibi harusi,hualika tu marafiki wa karibu hasa wa familia hivyo kulazimika kufuata ombi hilo.

Muhtasari

• Akiongea kwenye video ya YouTube baada ya malipo ya mahari, Bahati aliomba msamaha kwa marafiki waliokuwa wamefungiwa nje ya sherehe.

• "Nataka kuchukua wakati huu kuomba msamaha kwa marafiki wa Diana, marafiki zangu, kwa kutoalikwa. Kwa bahati mbaya, nilisikia, kwa ruracios, wazazi wa bibi arusi huchagua watakao hudhuria. Ombi kutoka kwa baba yetu lilikuwa kwamba hatutaki wageni.

Kevin Kioko anayejulikana kama Baha hisani: Instagramu
Kevin Kioko anayejulikana kama Baha hisani: Instagramu

Mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati ameeleza sababu ambazo zilimfanya kuzuilia marafiki kuhudhuria  hafla ya kitamaduni ya ndoa.  

Bahati aliwafungia nje baadhi ya marafiki wa Diana Marua kuhudhuria sherehe ya ndoa yao ya kitamaduni.

Akiongea baada ya kulipa mahari, Bahati aliomba msamaha marafiki waliokuwa wamefungiwa nje ya sherehe.

Bahati  alielezea kuwa hawakuweza kualika kila mtu kwa sababu baba ya Diana hakutaka watu wengi ila watu wa familia tu.

Afafanua kuwa kulingana na tamaduni,wazazi wa bibi harusi,hualika tu marafiki wa karibu hasa wa familia hivyo kulazimika kufuata ombi hilo.

"Nataka kuchukua wakati huu kuomba msamaha kwa marafiki wa Diana, marafiki zangu, kwa kutoalikwa. Kwa bahati mbaya, nilisikia, kwa ruracios, wazazi wa bibi arusi huchagua watakao hudhuria. Ombi kutoka kwa baba yetu lilikuwa kwamba hatutaki wageni.

Hata hivyo aliwatia moyo mashabiki wake na kuwaambia wasubiri mwaliko wa harusi yenyewe ambayo inatarajiwa hivi karibuni.

"Kama ni mwaliko utasubiri harusi nyeupe,"Alisema Bahati.

Mwimbaji huyo alimlipia mkewe mahari katika hafla ya kitamaduni iliyofanyika katika nyumba ya babake Diana Marua Joseph Omach.

"Ni rasmi !! hatimaye nimefanya malipo ya maadili ya Diana Marua na baba yake ametubariki kuendelea na mipango ya harusi💑."

Aliongeza kuwa,mkewe Diana hakuwa anatarajia haya yote ila alikusudia kutekeleza hayo kabla ya maadhimisho ya miaka saba wakiwa kwenye ndoa.

"Diana hakutarajia hili lakini nilikuwa na hamu sana ya kutekeleza haya  kabla ya maadhimisho  rasmi  ambayo no Octoba 20 mwaka huu,"Bahati aliandika haya kwenye kurasa za mitandao baada ya sherehe za kulipa mahar.

Mwanamuziki huyo aliongeza kuwa anakusudia kualika wageni 3000 kwenye harusi yake na kuahidi kutangaza tarehe kabla ya maadhimisho ya miaka saba ya ndoa.