Eric Omondi achangisha Sh556K kumsaidia mchuuzi wa mayai na smokie aliyevamiwa na kanjo

Eric Omondi alichangisha kiasi hicho cha pesa ndani ya saa 3 tu za kuwaongoza Wakenya kutuma michango yao huku akiwa live na huyo mrembo.

Muhtasari

• Picha za kutia huruma zilionesha jinsi Kanju walitawanya mtaji wa mrembo huo ambao ni pamoja na mayai, smokie na kachumbari kwenye lami.

Mchuuzi aliyeharibiwa mtaji na kanjo aokolewa na Eric Omondi
Mchuuzi aliyeharibiwa mtaji na kanjo aokolewa na Eric Omondi
Image: Instagram

Mwanaharakati wa haki za binadamu Eric Omondi kwa mara nyingine tena amewaongoza Wakenya mitandaoni kumchangishia hela ndefu mchuuzi wa mayai, smokie na kachumbari ambaye alitrend jana kufuatia shambulio la askari wa kaunti ya Nairobi kweney biashara yake.

Baada ya Wakenya wengi kujitokeza mitandaoni kulaani kitendo cha kanjo kuharibu mtaji wa mrembo huyo aliyetambulika kama Quinter Adhiambo, Omondi aliweka ujumbe kwamba alikuwa anamtafuta ili kumpa faraja kipindi hicho cha ukungu mwingi machoni mwake.

Hatimaye alimpata na katika kipindi cha saa 3 kuwaongoza Wakenya mitandaoni, Omondi aliweza kuchangisha Zaidi ya nusu milioni kwa ajili ya kukwamua biashara ya Adhiambo.

“WAKIANGUSHA TUNAINUA!!! Jana usiku tulifanikiwa Kuchangisha Ksh 556K ndani ya saa 3 kwa Quinter baada ya Halmashauri ya Jiji kumpiga teke kwa njia ya aibu na kuwaangusha chini. Alichomaanisha shetani kumvunja Mungu alikitumia KUINUA,” Omondi aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram Alhamisi asubuhi.

Omondi alimshukuru Mungu na watu ambao waliweza kuitikia wito wake wa kuchangisha kwa ajili ya mrembo huyo, baada ya picha za kutia huruma jinsi kanjo walimwaga na kutawanya mtaji wake kuenea mitandaoni.

“MUNGU ANASHINDA!!! Tutabadilisha maisha yake kabisa,” Eric aliahidi.

Hii si mara ya kwanza kwa Omondi kuchangisha michango kwa ajili ya Wakenya wanaotaabika.

Miezi michache nyuma, aliongoza wakenya kumchangishia mtoto aliyekuwa mgonjwa ambaye baada ya kucnagisha zaidi ya milioni moja, kwa bahati mbaya mtoto huyo aliangamia kwa ugonjwa.