Ukisema sitahubiri juu sina masomo, nakujibu nilitahiriwa mbele yako - Pasta Ng'ang'a achemka

“Kuna devil worshipper hapo Nairobi, na mnaijua mahali iko, na hamjafunga, hamjauliza hiyo," Ng'ang'a aliuliza.

Muhtasari

• Ng’ang’a anajipiga kifua akisema kwamba yeye alianza kuhubiri 1989.

Pasta Ng'ang'a
Pasta Ng'ang'a
Image: Screengrab//SasaTV

Mchungaji mweye utata James Ng’ang’a amewajibu kwa ukali wale wanaotaka kuwasilishwa kwa hoja ya kuwazuia wahubiri wote wasio na mafunzo ya thelojia kuhubiri nchini Kenya.

Ng’ang’a ambaye alikuwa anahubiri kwenye kanisa lake alisema kwamba wale wanaopiga vita wahubiri kisa hawana masomo wengi wao ni wenye masomo ambayo hayawasaidii, akisisitiza kwamba wasomi ndio chanzo kikubwa cha matatizo mengi yanayoikumba dunia ya leo.

Ng’ang’a alisuta hoja hiyo akisema kwamba wanaotaka kufungwa kwa makanisa halali yanayoongozwa na wahubiri wasio na masomo kwanza wanafaa kunyoosha mkono wao mrefu wa marufuku kwa makanisa ya itikadi za kiganga na kichawi, akisema kwamba wanajua vyema kwenye madhehebu hayo ya nguvu za kishetani yaliko.

Ng’ang’a anajipiga kifua akisema kwamba yeye alianza kuhubiri 1989 wakati hao wanaotaka sasa kanisa lake lifungwe walikuwa shuleni kufukuzia ‘makaratasi’ ambayo sasa yamewapa kiburi.

“Unajua mimi nimetoka na hii injili 1989, na nikihubiri nyinyi mnataka kuniambia sitahubiri, kipindi hicho mlikuwa shule mkisomea hayo makaratasi. Na msifikiri mimi mtanitisha, muweke mipaka sababu kuna waganga na wachawi na mnawajua mahali wako,” Ng’ang’a akisema.

“Kuna devil worshipper hapo Nairobi, na mnaijua mahali iko, na hamjafunga, hamjauliza hiyo, mnajua hayo madhehebu kule yako na hamwezi mkagusa hayo. Mnajua waganga na wachawi kule wako lakini hamzungumzii hao,” aliongeza.

Mchungaji huyo alisema kwamba iwapo kuna mtu yeyote anayetaka apigwe marufuku kutohubiri kwa kigezo cha masomo basi atamenyana naye kwa mwaka wa kutahiriwa, akijipiga kifua kwamba alitahiriwa mbele Zaidi ya wengi wa wale wanaotaka apigwe marufuku kuhubiri.

“Lakini ikifika ati ni mimi Ng’ang’a, sitahubiri eti kwa sababu sina masomo, basi nilitahiriwa mbele yakom, 1972. Wewe ulitahiriwa lini?” Ng’ang’a alitoa changamoto.