Willy Paul atenganisha mbivu na mbichi kuhusu video akimpa mrembo lift barabarani

Muhtasari

• “Kijana mwenye alirekodi hiyo video alikuja kunibembeleza kwa dirisha akisema yeye ni shabiki wangu kumbe alikuwa anachukuwa content." Pozee.

Willy Paul
Willy Paul
Image: Instagram

Wikendi iliyopita kulikuwepo na video iliyovuma mitandaoni ikionesha gari la msanii Willy Paul katika barabara ya Thika akimbeba mrembo.

Video hiyo ilienezwa wengi wakiichukua nje ya muktadha na kuhisi kwamba msanii huyo alikuwa ameendea mrembo wake na kumchukua lakini msanii huyo amejitokeza kutenganisha uongo na ukweli kuhusu yote yaliyosemwa kuhusu video hiyo.

Pozee alikiri kwamba ni kweli gari lilikuwa lake na kwamba ni vibaya kwa wengi kudhani kwamba akiwa msanii hafai kuwa na marafiki wa kike.

Msanii huyo alisema hata hivyo kwamba mrembo yule si rafiki yake bali ni rafiki wa rafiki yake aliyekuwa ndani ya gari na hivyo kuwataka watu kukoma kutumia picha na video za watu nje ya muktadha kabla ya kupata pande zote za hadithi.

“Ni kitu cha ujinga chenye hata sifai kuzungumzia lakini kwa sababu kipo pale nje acha nikielezee. Kwa hiyo ina maana kwamba mimi nikiwa celeb sifai kuwa na marafiki wa kike? Kwa sababu  venye waliiweka, walioanisha kimapenzi Zaidi kitu cha kushangaza huyo mrembo na mimi hatujuani. Ni rafiki wa rafiki yangu huyo alikuwa kwa gari,” Pozee alisema.

Alioneshwa kukerwa na kitendo cha aliyerekodi tukio lile akisema kwamba hata anahofia mrembo huyo anaweza anza kufuatwa na wakora wakidhani kwamba kitendo chake kuonekana na Willy Paul moja kwa moja ana pesa.

“Kijana mwenye alirekodi hiyo video alikuja kunibembeleza kwa dirisha akisema yeye ni shabiki wangu kumbe alikuwa anachukuwa content. Akarekodi mtoto wa wenyewe akiingia hapo, sasa hata maisha ya huyo mrembo sijui kama ako safe, wakora wanaweza kumkimbiza wakidhani ako na chapaa, juu unajua tena ukitembea na mimi watu wanajua uko na kitu,” alisema.