Mkewe Guardian Angel atunukiwa na UN kwa kufanya kazi nao zaidi ya miaka 20

Musila mwenye umri wa miaka 53 amefanya kazi kwenye shirika la UN kwa miaka 22 na mwaka jana walifunga harusi na mpenzi wake Guardian Angel wa miaka 33.

Muhtasari

• "Leo nilibahatika kuwa miongoni mwa wafanyakazi waliotunukiwa Tuzo za Utumishi Mrefu. " Musila alisema.

Esther Musila
Esther Musila
Image: Instagram

Esther Musila, mkewe mwanamuziki wa injili Guardian Angel ametunukiwa na shirika la umoja wa kimataifa UN kwa kuwa mmoja wa watu waliofanya kazi kwenye shirika hilo kwa miaka mingi Zaidi.

Musila kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia picha akiwa ameshikilia bango la utambulisho kutoka UN na kufichua kwamba alipewa tuzo hiyo ya utambulisho kwa kufanya kazi UN kwa Zaidi ya miaka 20 na bado anaendelea.

Musila alichukua fursa hiyo kujishukuru mwenyewe kwa kuwa mwaminifu kwa shirika la UN kwa kipindi hicho chote na kusema kwamba ana Imani kuu kwamba amefanya makubwa ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa muda huo.

“Imekuwa miaka 22 ya huduma kwa Binadamu. Leo nilibahatika kuwa miongoni mwa wafanyakazi waliotunukiwa Tuzo za Utumishi Mrefu. Utukufu na heshima zote kwa Mwenyezi.”

“Miaka 22 na bado inahesabika.... Ninataka kujishukuru kwa uaminifu wangu usioyumba kwa Umoja wa Mataifa na kuamini kwamba nimetoa michango yenye matokeo katika wajibu wangu wa huduma. Nakushukuru Esther. Mungu amekuwa mwaminifu kweli,” Musila alisema.