Diamond atakiwa kupima DNA ya mwanawe na Hamisa hadharani na majibu yatolewe wazi

Wiki iliyopita Diamond aliburuzwa mitandaoni kwa kuwaunganisha wanawe kutoka kwa Tanasha na Zari lakini akamtenga mwanawe na Hamisa.

Muhtasari

• "Ila this time anataka sehemu (Lab) itakayofanya hiyo DNA iwe public na matokeo ya DNA yapostiwe public" Hamisa alidaiwa kusema.

Diamond na Hamisa
Diamond na Hamisa
Image: Instageam

Mwanaharakati wa mitandaoni kutoka Tanzania Mange Kimambi amefichua kile alichokisema kuwa ni mazungumzo ya kina na mjasiriamali Hamisa Mobetto kuhusu ishu nzima ya mwanawe Dylan na kutengwa na baba yake Diamond Platnumz.

Kimambi anadai kwamba alimsihi Hamisa kukubali vipimo vya DNA kufanywa ili kuhakiki kama kweli Diamond ni baba mzazi kwa mwanawe kwa mara nyingine, ila safari hii majibu yawe ya hadharani.

Kimambi anadai kwamba mwanzoni, Hamisa alikataa jambo hilo alionekana kukubali hatima kwamba Diamond ameshaamua kumtenga mwanawe waziwazi na hivyo amemuachia mungu.

Hamisa anasema amemkabidhi mtoto wake kwa Mungu, Mungu ndio atakaemlelea mtoto wake na anasema kuna sababu Mungu kamwinua kimaisha ni ili aweze kumlea mwanae bila kupigizana kelele na baba mtu,” Mange Kimambi alisema.

Hata hivyo, baada ya kumbembeleza kwa muda, Kimambi alisema hatimaye Hamisa alikubali mwanawe kufanyiwa DNA kwa mara nyingine ila kwa sharti moja – mchakato mzima kufanyika katika maabara ya hadharani na majibu kutolewa wazi kwa umma.

“Nikamwambia Hamisa hapana, hili jambo sasa hivi limekuwa lakitaifa ndio umemwachia Mungu ila for the sake of your fans una obligation ya kukubali hii DNA irudiwe. Hamisa alinijibu na kusema sawa atafanya DNA ingine nchi yoyote mtakayotaka nyinyi wananchi ila this time anataka sehemu (Lab) itakayofanya hiyo DNA iwe public na matokeo ya DNA yapostiwe public, yaachiwe kwa taifa zima. Hataki tena kufanya private DNA inayosimamiwa na malawyer anataka DNA iwe public ili kusiwe na mjadala tena baada ya hapo,” Kimambi alidokeza.

Katika wiki mbili zilizopita, Diamond alisutwa vikali mitandaoni baada ya kuwakutanisha wanawe kutoka kwa Zari na Tanasha na kwenda nao nchini Rwanda lakini akamtenga mwanawe na Hamisa.