•Mbali na kumzawadi Tuzo za bei ghali Bahati ametanja kuwa anapanga kufanya harusi ya kifahari ambayo ametanja itakuwa bora zaidi kuwahi kufanyanyika nchini
Hivi majuzi mwanamuziki Bahati amevuma kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kumzawadi mkewe Diana zawadi mbali mbali wakati walipoadhimisha miaka saba ya ndoa.
Baada ya mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu msanii Bahati alisimulia kuwa alitumia shilingi millioni 30 kwa zawadi zote alizopeana kwa mke wake siku za kusherekea safari yao ya ndoa.
"Nilitumia muda wangu kufanikisha zawadi zangu kwa mke wangu sikufanya hivyo ili kujigamba ila ni kwa upendo kutoka roho yangu kwa kuwa mke wangu Diana amekuwa wa maana sana kwa familia yetu kwa upendo na ukarimu wake ndio maana millioni 30 kufanikisha zawadi zake ni kwa upendo wangu kwake,"alisema.
Baadhi ya zawadi alizomtunuku mke wake Diana ni gari la kifahari aina ya Range Rover lenye dhamani ya millioni kumi na tisa, zawadi hiyo iliadamana na sherehe za kitamaduni ambazo mwanamuziki huyo alienda kumlipia mkewe mahari.
Kwenye mahojiano hayo Bahati ametaja mipango yake kufanikisha harusi bora zaidi kuwahi kufanyika nchini akisema itakuwa ya aina yake.