Rema ashambuliwa na mashabiki kwa video yenye taswira ya 'kishetani'

Mashabiki walifurika kwenye chapisho hilo Instagram na wengi walionekana kuuliza swali hilo hilo la taswira nzima ya kishetani.

Muhtasari

• “Wewe pia? Kitufe cha kuacha kukufuata mara moja,” Lelatokgatle alisema.

• “Ninaomba damu ya Yesu kwenye chapisho hili. Mungu apishe mbali. nakukemea. Kukuza upuuzi, mbona hufai kuwa Malaika?” THEREALNEDU alisema.

Rema
Rema
Image: Instagram

Wiki chache  baada ya kugeuka gumzo baada ya kufungiwa kutotumbuiza nchini Ethiopia kutokana na mkufu wake uliotiliwa shaka na mamlaka kwa kuhusishwa na itikadi za kichawi, msanii Rema kutoka Nigeria kwa mara nyingine tena amejipata kwenye skendo sawia.

Wakati huu, video yake ya hivi punde ya muziki imeitwa. Kijisehemu cha taswira za hivi punde zaidi za Rema zilizoshirikiwa kwenye ukurasa wake zilizotambulishwa kama Smooth Criminal kimeibua hisia kubwa.

Katika klipu hiyo ambayo Rema ameionjesha kama kionjo cha ngoma mojawapo kutoka kwa albamu yake atakayoiachia Ijumaa hii, Rema alionekana akiwa kwenye ukumbi wenye kuta za rangi nyekundu huku mwenyewe akiwa kama giza asiweze kuonekana vizuri.

Hata hivyo, kilichowazuzua mashabiki wake ni jinsi picha na muonekano wake kwenye klipu hiyo ulivyohaririwa na kutoa taswira ya kishirikina.

Rema alionekana anakengeuka kwa nywele zilizochomoza kama mishale kichwani huku mikononi akiwa amevalia vazi refu jeusi lenye mifano ya vidole kadhaa na pia kwa wakati Fulani picha hiyo ilikuwa inahaririwa kwa kuvutwa hadi kuonekana kama mabaki ya mifupa ya binadamu.

Mashabiki walifurika kwenye chapisho hilo Instagram na wengi walionekana kuuliza swali hilo hilo la taswira nzima ya kishetani.

Ilipigiwa kelele kama ya uchawi na kejeli ya mitetemo ya kishetani. Wengi waliendelea kutambua kwamba aina ya ukuaji ambayo mwimbaji mchanga ameshuhudia hivi karibuni inaweza tu kuhusishwa na ushirika wake na kikundi cha uchawi cha ulimwengu wa kiza.

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, Rema ameshinda tuzo nyingi zaidi za ndani na kimataifa kama mwimbaji wa Nigeria. Alitawala tuzo za mwisho za Headies. Ambapo alishinda gongo nne usiku na pia hivi majuzi kwenye tuzo za kwanza kabisa za Trace nchini Rwanda, Rema alishinda.

Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa mashabiki wake kuhusiana na chapisho hilo;

“Ni mimi au naona taswira za kishetani,” Simply Nyasha aliuliza.

“Kwa nini mwonekano mzima wa kishetani?” Official Prince Koko aliuliza.

“Wewe pia? Kitufe cha kuacha kukufuata mara moja,” Lelatokgatle alisema.

“Ninaomba damu ya Yesu kwenye chapisho hili. Mungu apishe mbali. nakukemea. Kukuza upuuzi, mbona hufai kuwa Malaika?” THEREALNEDU alisema.

Maoni yako ni yepi?