Rema afichua ukweli wote kuhusu kudaiwa kuwa mwanachama wa illuminati

"Ninapoendelea, utekelezaji wangu utabadilika bila msamaha. Tafadhali mjue msanii wako. Ndio maana nafanya mahojiano,” alimaliza katika kutoa kero lake.

Muhtasari

• Rema alisema kuwa anafanya kazi kwa bidii ili kutengeneza muziki wa hali ya juu na anatarajia mashabiki wake kutoa sifa inapostahili badala ya illuminati.

Rema
Rema
Image: Instagram

Mwimbaji maarufu wa Nigeria Divine Ikubor anayefahamika kwa jina la Rema hatimaye amesafisha hali ya hewa kufuatia tetesi zilizoenea kuwa alijiunga na illuminati hivi karibuni.

Katika chapisho lililoshirikiwa kupitia sehemu ya insta-story za ukurasa wake wa Instagram uliothibitishwa leo, Oktoba 25, 2023, Rema alizungumzia nadharia za njama za Illuminati na njama zingine kwamba ameuza roho yake kujiunga na jumuiya hiyo inayotajwa kuwa yenye itikadi kali za utoaji damu.

Alikanusha kabisa uhusiano wowote na jamii ya siri na akathibitisha kwamba kujitolea kwake kumekuwa kwa sanaa yake tangu mwanzo.

“Na uvumi kuhusu illuminati ni upuuzi mtupu, ninafanya kazi kwa bidii sana ili kuwatungia mashairi na nyimbo nzuri mashabiki wangu na nyinyi kuanza kupaisha hadithi za kipuuzi, ua fikira hizo sasa. Siku zote Yesu ni mfalme,” alisema.

Rema katika chapisho hilo aliwataka mashabiki wake wa tangia siku ya kwanza wanaojulikana kama Ravers kuwaelimisha Ravers wapya kuhusu historia na urithi wake, kuangazia rangi kuu za utamaduni wake na umuhimu wa vipengele fulani nchini Benin.

"Day 1 Ravers, saidia kuelimisha Ravers wapya ambazo nimekuwa kwenye shit hii kwa muda mrefu. Ningekuwa na uwazi zaidi ikiwa uta Google kwa urahisi ninakotoka, rangi kuu za urithi wangu ni nini, nini kinachoruka katika anga ya Benin kila jioni, nk,” aliongeza.

Rema alisema kuwa anapoendelea kama msanii, mbinu yake ya kisanii pia itapitia mageuzi. Alisisitiza kujitolea kwake katika kuunda sanaa ambayo inaunganisha kwa kina na watazamaji wake huku akikataa madai yoyote kwamba mafanikio yake yanahusishwa na nguvu zisizo za kawaida.

Rema alisema kuwa anafanya kazi kwa bidii ili kutengeneza muziki wa hali ya juu na anatarajia mashabiki wake kutoa sifa inapostahili badala ya illuminati anazozitaja kuwa za kishetani.

"Ninapoendelea, utekelezaji wangu utabadilika bila msamaha. Tafadhali mjue msanii wako. Ndio maana nafanya mahojiano,” alimaliza katika kutoa kero lake.

Rema Illuminati
Rema Illuminati

Hivi majuzi, Rema aliburuzwa mitandaoni baada ya kuachia kionjo cha EP yake mpya ambayo inatoka leo Ijumaa lakini kilichowafanya mashabiki wengi kuzungumza ni uhariri wa hali ya juu uliofanywa kwenye video ya kionjo hicho kutoa taswira ya picha zilizotajwa kuwa za kishetani.