Shule yangu itakuwa mume wangu, mapenzi nimeachia mabinti zangu - Akothee

"Shule hii itakuwa mume wangu kusema kweli, nitajitolea pakubwa kuhakikisha kwamba ninawapa watoto kile wanachohitaji kufaulu kimasomo. Mapenzi nimeachia watoto wangu,” Akothee alisema.

Muhtasari

• Hata hivyo, alisema kwamba watu wakumbuke kwamba yeye sim awe kwani kuna kipindi atafika atahitaji mapenzi.

Akothee
Akothee
Image: Instagram

Licha ya awali kufunguka kwamba bado yuko sokoni kutafuta mapenzi, msanii Akothe ameonekana kuchukua mkondo tofauti wa kifikira na kimawazo akisema kwamba mapenzi ameachia mabinti zake.

Mjasiriamali huyo ambaye juzi amefurahia kusajiliwa kwa shule yake ya Akothee Fundation Academy, alisema kwamba kinachomfanya kusitisha suala la kuhangaishwa na mapenzi ni kwa sababu anataka kuwekeza nguvu zake zote katika ufanisi wa shule hiyo.

Alisema kwamba atajitoa kwa hali na mali katika ufanisi wa shule hiyo kiasi kwamba itakwua ndio mume wake.

“Mimi na mapemzi aki sijui ni nini nitasema, hiyo kitu haingiani vile nataka, sidanganyi. Nafikiri nimeshikika sana kimawazo. Sijielewi. Shule hii itakuwa mume wangu kusema kweli, nitajitolea pakubwa kuhakikisha kwamba ninawapa watoto kile wanachohitaji kufaulu kimasomo. Mapenzi nimeachia watoto wangu,” Akothee alisema.

Hata hivyo, alisema kwamba watu wakumbuke kwamba yeye sim awe kwani kuna kipindi atafika atahitaji mapenzi.

“Lakini kumbuka mimi si mawe, nina homoni na damu inayotembea katika huu mwili. Siwezi achia mtu uhusiano, niachie mtu uhusiano kwa nini,” Akothee alijichanganya kwa mara nyingine.

Awali tuliripoti kwamba Akothee aliweka bayana mpango wake wa kutoachia mapenzi licha ya kuwa na umri Zaidi ya miaka 40.

“Kama haitakwenda jinsi nilivyotarajia tena tunarudi, kama ambavyo niliwaambia mimi siondoki sokoni, mimi ndio soko mwenyewe. Mbona niondoke soko langu, tunakanyagana tu hapo,” Akothee aliongeza.

"Na nimerudi vile mnaona mimi bado wa moto. siwezi ondoka sokoni, nilisonga tu kando kidogo. soko ni hapo hapo tunaoga na tunakaukia hapo," alisisitiza.