Siondoki sokoni mimi mwenyewe ndio soko, nilisonga kando kidogo na nimerudi - Akothee

"Nilikutana na mamake Omosh nilimwambia kwamba mimi ni mama wa watoto 5 na nimekuwa katika mahusiano mengi yaliyofeli kwa hiyo jua mvulana wako ndio anafuata,” alisema.

Muhtasari

• Pia alikanusha madai kwamba Omosh ni kijana kutoka Pakistan, akisema kwamba ni wa Uswizi na hata walikutana huko na mamake pia.

• "Na nimerudi vile mnaona mimi bado wa moto. siwezi ondoka sokoni, nilisonga tu kando kidogo. soko ni hapo hapo tunaoga na tunakaukia hapo," alisisitiza.

wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Akothee na mumewe Denis Shweizer wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Licha ya kuwa na umri wa miaka Zaidi ya 40, msanii na mjasiriamali Akothee amesisitiza kwamba hayuko tayari kuachana na suala la kutafuta mapenzi.

Akothee amesema haya licha ya kwamba pia hajakuwa na bahati ya kupata mwanamume wa kudumu naye kwa muda mrefu, wa hivi karibuni akiwa mpenzi wake kutoka Uswizi ambaye alivunja ndoa yao miezi 5 tu baada ya harusi ya kifahari.

Akothee anasisitiza kwamba hataondoka sokoni muda wowote kwani yeye mwenyewe ndiye soko na atazidi kusukuma hadi pale nyota yake itakaposimama.

“Kama nilivyowaambia awali, ukishafikisha miaka 40, baadhi yenu ni wadogo kiumri, unatashangaa jinsi Akothee anavyosahau kuvunjwa moyo haraka hivyo. Mimi niko na majukumu mengi ya kutekeleza. Huwa sifanyi maamuzi kwa kuzingatia njaa, maamuzi yangu yanazingatia hisia wakati huo,” alisema.

“Mimi nilikuwa nimezama kwenye mapenzi kusema ukweli, na nilikuwa nimepata pacha wangu, mbona nisifunge ndoa na yeye? Kama haitakwenda jinsi nilivyotarajia tena tunarudi, kama ambavyo niliwaambia mimi siondoki sokoni, mimi ndio soko mwenyewe. Mbona niondoke soko langu, tunakanyagana tu hapo,” Akothee aliongeza.

"Na nimerudi vile mnaona mimi bado wa moto. siwezi ondoka sokoni, nilisonga tu kando kidogo. soko ni hapo hapo tunaoga na tunakaukia hapo," alisisitiza.

Pia alikanusha madai kwamba Omosh ni kijana kutoka Pakistan, akisema kwamba ni wa Uswizi na hata walikutana huko na mamake pia.

“Omosh ni Mswizi anatoka katika familia iliyochanganyika. Mamake ni singo ana watoto 5, yeye ni mzawa wa pili. Nilikutana na mamake wakati tulienda Italia, alifurahia kunijua niliongea na yeye kwa Kijerumani na nilimwambia kwamba mimi ni mama wa watoto 5 na nimekuwa katika mahusiano mengi yaliyofeli kwa hiyo jua mvulana wako ndio anafuata,” alisema.