Mikakati ya kuzindua Studio ya kisasa yenye jina Ally B imeanza Aisha Jumwa asema

Muhtasari

•Ally B anafahamika sana kwa nyimbo zake maarufu kama vile ‘Maria’ na ‘Bembea’.

• Alifariki katika hospitali ya Coast General Teaching and Referral Hospital mjini Mombasa Jumatano alasiri ambapo alikimbizwa baada ya kulalamika kuhisi maumivu.

Image: Aisha Jumwa atangaza mikakati ya kizindua studio ya kisasa yenye jina Ally B

Waziri wa jinsia Aisha Jumwa ametagaza mikakati ya serikali kuzindua studio ya kisasa ya  kurekodi muziki kwa wanamuziki wanaochipuka kama kumbukumbu ya msanii Ally B.

"Msanii Ally B ni kioo cha jamii nyimbo zake zilipedwa na wengi, aliwasaidia wasanii wengi kurekodi nyimbo kwa ajili ya kutoa shukrani kwake na kumbukumbu kwa kwa maisha  yake  tutajenga studio ya kisasa yenye Lebo Ally B,"alisema waziri.

Jumwa  ambaye alimwakisha Rais William Ruto alitangaza haya wakati wa hotuba yake huku akipeana mchango wa Rais  Ruto wa nusu millioni  kufariji familia na mchango wake wa laki moja.

Mwanamuziki  huyu mkongwe mzaliwa wa pwani Ali Khamisi Mwaliguli almaarufu Ally B alifariki siku ya Jumatano alipokuwa akikimbizwa katika hospitali ya Coast General mjini Mombasa.

Ally B iliripotiwa kwamba alikuwa na ugonjwa wa nimonia kwa siku kadhaa, kaka yake Mohamed Ramadhan alifichua.

Marehemu alifanyiwa ibada ya mazishi ya Kiislamu kabla ya mwili wake kuzikwa katika eneo la Maziara ya Cobra katika mtaa wa Mishomoroni, Kaunti ya Mombasa.

Watu mashuhuri, wanasiasa, mashabiki ni miongoni mwa walioungana na familia, majirani na marafiki wa marehemu mwimbaji huyo kumzika.