Stevo Simple Boy atangaza kuokoka baada ya kusikiliza ngoma ya Christina Shusho

Stevo kupitia Instagram alipakia video akisikiliza wimbo huo huku akimshukuru Asila kwa mistari mizuri ya kumtukuza Mungu na hata kusema kwamba wimbo huo ulimbariki pakubwa.

Muhtasari

• “Mimi sana sana napenda kuhimiza jamii ambayo ni kuwapatia ujumbe, siimbi ngoma za kupotosha watu,” alisema.

• Stevo alituma ujumbe kwa msanii huyo akiomba nafasi ya kuweka mistari yake ya injili katika remix ya wimbo.

Shusho amchochea Stevo kuokoka
Shusho amchochea Stevo kuokoka
Image: insta

Msanii wa rap kutoka Kibera, Stevo Simple Boy ametangaza kupata wokovu baada ya kuchochewa na wimbo wa msanii Bunny Asila akimshirikisha malkia wa injili kwa muda mrefu kutoka Tanzania, Christina Shusho.

Stevo kupitia Instagram alipakia video akisikiliza wimbo huo huku akimshukuru Asila kwa mistari mizuri ya kumtukuza Mungu na hata kusema kwamba wimbo huo ulimbariki pakubwa.

Stevo alituma ujumbe kwa msanii huyo akiomba nafasi ya kuweka mistari yake ya injili katika remix ya wimbo.

Hii ngoma ya Nakuja ya Bunny asila akishikisha @christinashush imenigusaaa sàaaaana 🥺 ningeomba wanipa vesi tuipige RMX ndugu yangu @asilabunn ukiona huu ujumbe kuja tuonge @officialchristi pia ameua,” alisema Stevo.

Alingeza kwamba kufuatia ujumbe wa wimbo huo wa kugusa, alisema kwamba ameamua kuokoka rasmi na kuanza kutoa mizki ya injili.

“Hio ngoma ya Bunny asila na Christina shusho ndio imefanya niokoke ....#nakuja mambo Iko murwa murwa 😊” aliongeza.

Hivi majuzi, Stevo Simple Boy alisema kwamba nyimbo zake anazoziimba ni tofauti na wengine, kwani yeye anazingatia katika ujumbe wa kutoa motisha au kuhimiza au kutoa funzo katika jamii, huku akishindwa kubainisha kama ni msanii wa sekula au injili.

Alikuwa anajilinganisha na wasanii wengi wa Kenya, amabo kulingana naye, wengi wanaimba nyimbo kwa kuegemea mapenzi sana kwa kutumia lugha chafu, akisema kwamba si lazima msanii aimbe lugha chafu ili kutambulika kwenye Sanaa.

Mimi sana sana napenda kuhimiza jamii ambayo ni kuwapatia ujumbe, siimbi ngoma za kupotosha watu,” alisema.

“Unajua si kila mtu huwa anataka kusikiliza ngoma za hepi moments za kusisimua mwili hapana, mle ndani kuna wazee, kuna wale watu wazima, imbeni ngoma ambayo hata ukiwa pale kwa nyumba unaweza kusikiliza hata na mzazi,” aliongeza.