Diamond kukutanishwa na 'role model' wake wa mavazi, Asake kwenye jukwaa moja

Licha y Diamond kuwa na muda mrefu kwenye tasnia ya Asake akiwa kama chipukizi, wamekuwa wakihusishwa sana katika mfanano wa mavazi, mitindo ya nywele na hata kutembea.

Muhtasari

• Tangazo la wawili hao kujumuishwa kwenye tamasha hilo lilizua minong’ono mingi kutoka kwa mashabiki wa Bongo Fleva.

Asake na Diamond
Asake na Diamond
Image: Instagram

Waandaaji wa tamasha la Afro Nations wametoa orodha rasmi ya wasanii wa Kiafrika ambao watatumbuiza kwenye tamasha hilo mwezi Juni mwaka ujao nchini Ureno.

Na katika orodha hiyo, kwa mara ya kwanza msanii Diamond Platnumz atakutanishwa na Asake, msanii anayekuja kwa kasi Zaidi kutoka nchini Nigeria ambaye kwa mara nyingi Diamond ametuhumiwa ku,uiga katika mavazi, mitindo ya nywele lakini pia hadi kutembea na vitu vingine.

Kwa upande wa wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva, mashabiki wengi wamekuwa wakisema kwamba msanii Diamond anamuiga sana Asake katika vitu vingi tu licha ya kwamba Asake hana muda mrefu kwenye tasnia na yeye Diamond amekuwa karibia miaka 15 kwenye muziki sasa.

Sasa tangazo la wawili hao kujumuishwa kwenye tamasha hilo lilizua minong’ono mingi kutoka kwa mashabiki wa Bongo Fleva ambao wanahisi kwamba hii itakuwa mara ya kwanza kuona nani mkali wao kwenye jukwaa.

Shoo hiyo itafanyika kuanzia tarehe 26 Juni mpaka tarehe 28 na baadhi ya majina makubwa ambao watatumbuiza ni pamoja na Rema, Asake, Ninho, Omah Lay, Mr Falvour, Diamond Platnumz, Tyla, Seyi Vibez, The Compozers, Odumodublvck miongoni mwa wengine.