Msanii David Wonder aeleza jinsi ugonjwa umeathiri muziki wake

Nimekuwa mgonjwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu -David Wonder

Muhtasari

• Mwanamuziki huyo aliezea masaibu yake huku akifichua kuwa kuna wakati mmoja alipitia magumu baada ya kupatana na wezi waliomuibia.

David Wonder
David Wonder
Image: Faceboook

Mwimbaji wa nyimbo za injili David Wonder amejitokeza hadharani na kusimulia jinsi ambavyo ugonjwa umemulemaza kwa muda jambo ambalo limeathiri afya yake na kusababisha uchungu mwingi ndani ya moyo wake.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu amekuwa akiugua na kupambana na hali ngumu ya maisha.

"Nimekuwa mgojwa kwa muda wa mwaka na nusu madaktari walionihudumia walinieleza kuwa huenda nikosea kuendeleza taaluma yangu ya muziki kwa kuwa mwili wangu ulihitaji kupumzishwa kwa muda bila ya kuimba na kupiga densi jambo hili kwangu limekuwa zito kwani liliharibu mipango yangu ya muziki,"alisema.

Kulingana na msanii huyo wa nyimbo za injili aliathirika kiafya kufikia kiwango cha kuvuruga kiwango chake cha ubunifu jambo ambalo amesema kwa sasa amejaribu kuchipua kipawa chake ila kwa upole kwa kuwa bado hajarudi katika hali ya kawaida.

"Najaribu kurudia kazi yangu ya muziki ila kwa kiasi kwa kuwa madaktari walinishawishi kutulia kwanza ndiposa mwili wangu uwe na nguvu,"alisema.

Mwanamuziki huyo aliezea masaibu yake huku akifichua kuwa kuna wakati mmoja alipitia magumu baada ya kupatana na wezi waliomuibia bidhaa zake.