Cardi B afichua kuwa analipisha sh.153 Milioni kwa shoo moja

Ingawa milioni 153 ni pesa nyingi sana, msanii huyo si mwanamuziki anayelipwa zaidi kwa hafla za maonyesho.

Muhtasari

• Nyota  huyo wa Hiphop alidhibitisha kwamba bei ya shoo zake ni ghali mnokwa mashabiki wa kawaida.

• "Siwezi  kutoka kwangu  kuenda kutumbuiza  ikiwa tikiti sio sh 153 milioni na zaidi Ikiwa mashabiki hawatalipa kiasi hicho basi sitoki,” 

CARDI B
CARDI B
Image: INSTAGRAM

Msanii  wa nyimbo za Hip-hop Belcalis Almanza  maarufu kama Cardi B ameeleza kiasi cha pesa mashabiki  wake wanazolipa wanapohudhuria shoo zake.

Nyota  huyo wa Hiphop alidhibitisha kwamba bei ya shoo zake ni ghali mnokwa mashabiki wa kawaida.

Mama huyo wa watoto wawili alifichua kwamba hangeweza kuondoka nyumbani kwake kwa tamasha ikiwa mwandalizi au promota hakuwa tayari kufikia tikiti ya  sh153 Milioni na zaidi.

"Siwezi  kutoka kwangu  kuenda kutumbuiza  ikiwa tikiti sio sh 153 milioni na zaidi Ikiwa mashabiki hawatalipa kiasi hicho basi sitoki,” alisema.

Hii si mara ya kwanza kwa nyota huyo kutangaza bei ghali ya show zake kwa mashabiki.

Mwaka jana, Cardi B alitumia akaunti yake ya X kwa kiasi kikubwa na kujivunia jinsi alivyotengeneza dola milioni 1 kwa onyesho la dakika 35 huko Miami.

Katika katika chapisho hilo la zamani, nyota huyo alieleza kuwa alitumbuiza takriban watu 400 katika hafla ya benki ya wasomi kabla ya kuwashauri watu wafikirie juu kuhusu gharama ya tikiti yake kabla hawajaanza kuzungumza naye kuhusu kufanya shoo.

""Nililipwa dola milioni 1 ili kutumbuiza katika hafla ya mwanabenki  mashuhuri." Hafla hiyo ilifanyika kwa "watu 400 na kwa dakika 35 tu,” alichapisha.

Mashabiki walikuwa wepesi kulinganisha tikiti yake na ile ya mpinzani wake Nicki Minaj ambaye watu wanaamini hutoza Ksh300,000 kwa kila onyesho.

Ingawa milioni 153 ni pesa nyingi sana, msanii huyo si mwanamuziki anayelipwa zaidi kwa hafla za maonyesho.

Orodha kubwa ya Wasanii kama Taylor swift na Kanye west hupata mabilioni kwa usiku mmoja haswa wanapokuwa kwenye ziara.