Manzi wa Kibera amtaka mpenziwe 67, kujitokeza kwa DNA baada ya kukana mimba

"Kuna uvumi mwingi ila nataka kuweka wazi kuwa mimi na mzee wangu tutarudiana na huyu mzee kwa maswala ya chumbani ni staa,"alisema.

Muhtasari

• Kuna uvumi mwingi ila nataka kuweka wazi kuwa mimi na mzee wangu niko na imani tutarudiana na huyu mzee kwa maswala ya chumbani ni staa.

Manzi wa Kibera na mpenzi wake wa zamani.
Manzi wa Kibera na mpenzi wake wa zamani.
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti Manzi wa Kibera amefunguka  kuhusiana na mpenziwe  ambaye ni mzee wa miaka 67 huku akimtaka kujitokeza ili wafanye DNA kwa kile anadahi kuwa mpenziwe huyo kwa muda amekuwa akikana Mimba yake.

Manzi wa Kibera kwenye mahojiano ya moja kwa moja aliweka wazi amekuwa kwa mahusiano mazuri na mpenziwe ila wakati alipompachika mimba alibadilika kwa kile alichokisema mpenziwe alianza kueneza uvumi kwenye mitandao akikana mimba hiyo.

"Kumbe si vijana pekee wanaruka mimba hadi wazee sasa huyu mzae wangu ni mtu wa kwenda kwenye mitandao akisema ati mimba si yake nashangaa wanaume ni wale wale tabia moja tu,hata nimechoka na wanaume lakini lazima mzae wangu ajitokeze tufanye DNA nimechoka kusemwa,"alisema Manzi wa Kibera.

Sosholaiti huyo kwenye mahojiano hayo alisimulia zaidi kuwa Mpenziwe amekuwa akimshuku kumsaliti kimapenzi na wanaume wengine jambo ambalo kulingana naye Mpenziwe alichochewa na adui zake.

Licha ya hayo  mwanasosholaiti alindokeza kuwa upendo wake kwa Mpenziwe huyo wa miaka 67 ni mwingi na iwapo atajitokeza kufanya DNA yuko tayari kufunga pingu ya maisha naye kwa kile alichodai kuwa mzee hodari kwa maswala ya chumbani.

"Kuna uvumi mwingi ila nataka kuweka wazi kuwa mimi na mzee wangu niko na imani tutarudiana na huyu mzee kwa maswala ya chumbani ni staa,"alisema.