Mwili wa msanii aliyekufa wasimamishwa wima ili mashabiki waupigie kwaheri (video)

Maiti yake ilikuwa imesimamishwa ndani ya kijumba cha glasi ukiwa umevalishwa kofia, saa, mavazi aliyopenda kuvalia, cheni kifuani lakini pia fimbo mkononi, kwa mbali ungedhani ni kinyago cha kuuza nguo kumbe ni maiti.

Muhtasari

• 2pm alikutana na kifo chake katika ajali mbaya iliyotokea Ijumaa, Novemba 17, huko Wassa Akropong, Mkoa wa Magharibi wa Ghana.

Mwili wa 2PM
Mwili wa 2PM
Image: TikTok

Kwa mara nyingine tena raia wa Ghana wamezua gumzo katika mitandao ya kijamii kuhusu utamaduni wa kuaga marehemu.

Kisa cha kushangaza ambacho kimezua mjadala pevu katika mitandao ya kijamii ni baada ya mwili wa msanii mmoja aliyefariki kwa ajali wiki iliyopita ulivyoagwa na umma na mashabiki wake.

Katika picha na video ambazo zimeenezwa kwenye mitandao ya kijamii, rapa huyo kwa jina 2pm alitolewa mochwari na kufikishwa nyumbani kwake lakini kabla ya maziko, mashabiki wake wakataka kumupa buriani kwa kuutazama mwili wake kwa mara ya mwisho.

Kwa kawaida aktika jamii nyingi, mwili hutazawa ukiwa umelalishwa ndani ya jeneza, lakini nchini Ghana hali ni tofauti; mwili wa kijana huyo uliondolewa mazima ndani ya jeneza na kuegemezwa kwa kusimamishwa wima huku watu wkaipita na kuutazama utadhani ni kinyago kilichokuwa kimevalishwa nguo.

2pm alikutana na kifo chake katika ajali mbaya iliyotokea Ijumaa, Novemba 17, huko Wassa Akropong, Mkoa wa Magharibi wa Ghana.

Maiti yake ilikuwa imesimamishwa ndani ya kijumba cha glasi ukiwa umevalishwa kofia, saa, mavazi aliyopenda kuvalia, cheni kifuani lakini pia fimbo mkononi, kwa mbali ungedhani ni kinyago cha kuuza nguo kumbe ni maiti.