Ssaru akiri muziki 'mchafu' ndio unauza huku akipandisha bei ya mahari hadi bilioni 1.5

"Ukitoa 1.5B hakuna haja kuuliza mimi naleta nini mezani, Nafikiri mimi naleta kila kitu kwa sababu katika haya maisha nakuja na mapenzi na mshahara yangu mwenyewe, nakuja na urembo, hivyo vyote.”

Muhtasari

• Ssaru alikiri kwamba yeye ni yule mrembo ambaye anaelewa akisema kwamba maisha yake penye yako hahitaji mwanamume mwenye hana hela.

Ssaru
Ssaru
Image: Facebook

Wiki mbili tu baada ya kuweka bi ya mahari yake kuwa shilingi za Kenya bilioni moja, rapa Sylvia Ssaru amepandisha bei hiyo na kusema kwamba kwa sasa inasimamia bilioni 1.5 huku akiwaambia wanaume kwamba wakizubaa bei itavuka bilioni 2.

Katika mahojiano na Mungai Eve mjini Eldoret wikendi iliyopita alikokuwa mmoja wa wasanii wa kutumbuiza kwenye tamasha la Love and Vibes lake Nadia Mukami na mpenziwe Arrow Bwoy, Ssaru pia aliweza kutoa sababu kadhaa tu ambazo zinamfanya kuhisi kabisa mahari yake si chini ya bilioni.

“Sasa hivi ni 1.5b na wakichelewa 2024 nitapandisha, wenye wanasema nitajioa mimi najimudu kwa hivyo kama kuna mtu lazima anioe, lazima akuwe Zaidi yangu yaani akuje na nyingi Zaidi yangu,” alisema.

Mrembo huyo alisema kwamba kwa wale wanauliza ataleta nini juu ya meza, alisema kwamba ukiachia mbali meza yeye ndio msingi wa nyumba yenyewe ambako meza itakaa.

Ssaru alikiri kwamba yeye ni yule mrembo ambaye anaelewa akisema kwamba maisha yake penye yako hahitaji mwanamume mwenye hana hela.

“Maisha yangu sasa hivi, sihitaji mwanamume kabwela, mimi nahitaji mtu mwenye pia anaweza niunga mkono na vitu vingine, nikichumbiana na mtu kabwela itanivuta nyuma. Ni mwanamume tu ang’ang’ane afike tu bei,” Ssaru alisema huku akifichua kwamba alijipata katika mtego wa kuchumbiana na mwanamume kabwela na alipogundua hata hakusubiri.

Kuhusu chenye atachangia kwenye ndoa baada ya kutolewa mahari ya bilioni na nusu, Ssaru alisema;

“Mimi ndio msingi wa hiyo nyumba nzima kwa hivyo achana na meza, mimi ni nyumba imekamilika. Sasa hivi unaulizwa unaleta nini nyumbani, sio meza sasa. Nafikiri mimi naleta kila kitu kwa sababu katika haya maisha nakuja na mapenzi na mshahara yangu mwenyewe, nakuja na urembo, hivyo vyote kama havitoshei juu ya meza sijui.”

Mrembo huyo alikubali kwamba mashabiki wengi wa Kenya wanapenda muziki wenye maudhui chafu lakini akasema kwamba yeye hafanyi muziki kwa sababu ya kupendwa kwa maudhui chafu bali anafanya kwa sababu ya matakwa ya mashabiki.

“Ni kweli muziki chafu huuza, hizo ndio ngoma Wakenya wanapenda, ukitoa uko na shoo hapa na kule. Lakini mimi natoa ngoma yenye mashabiki wanakubali na ile yenye wanaitishia Zaidi, sio ile yenye inauza sana,” alisema.