Koffi Olomide azuru Radio Jambo, na kuahidi shoo ya kumezea mate

Tikiti za mapema zinauzwa kwa Sh6,000, watakaonunua getini watalipa Shilingi 7,500 na VIP watalipa Sh25,000.

Muhtasari

• Mwanamuziki huyo wa rhumba/soukous alisema anashukuru kwa kupata fursa ya kurejea Kenya na kuonyesha kipawa chake.

Mtangazaji wa Radio Jambo Gidi, msanii wa rhumba Koffi Olomide, msimamizi wa mitandao ya kijamii ya Radio jambo Naom Mainye na mtangazaji Ghost Mulee katika studio za Radio Jambo, Lion Place Westlands mnamo Desemba 7, 2023. Picha: Brian Smith

Msanii maarufu kutoka DRC Koffi Olomide almaarufu Le Grand Mopao Mokonzi alitua Nairobi Desemba 6 kwa ajili ya tamasha la amani lililoandaliwa na Radio Africa Events.

Koffi atatumbuiza pamoja na wasanii wengine mnamo Desemba 9, 2023, kwenye Ukumbi wa ASK Dome, eneo la mainyesho ya Kilimo ya Nairobi.

Tikiti zinauzwa, na mashabiki wanaweza kuzipata kupitia ticketyetu.com.

Tikiti za mapema zinauzwa kwa Sh6,000, watakaonunua getini watalipa Shilingi 7,500 na VIP watalipa Sh25,000.

Afisa mkuu Mtendaji wa Radio Africa Group Patrick Quarcoo na Mwanamuziki Koffi Olomide wakiwa Lion Place Westlands mnamo Desemba 7, Picha: Brian Smith
Afisa mkuu Mtendaji wa Radio Africa Group Patrick Quarcoo na Mwanamuziki Koffi Olomide wakiwa Lion Place Westlands mnamo Desemba 7, Picha: Brian Smith

Mwanamuziki huyo wa rhumba/soukous alisema anashukuru kwa kupata fursa ya kurejea Kenya na kuonyesha kipawa chake.

"Nina furaha zaidi, na siwezi kusubiri kuwa jukwaani na kutumbuiza watu wa Kenya. Nina furaha sana kuwa hapa," alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Africa Martin Khafafa akizungumza na wanahabari katika afisi za Lion Place Westlands mnamo Desemba 7, Picha: Brian Smith
Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Africa Martin Khafafa akizungumza na wanahabari katika afisi za Lion Place Westlands mnamo Desemba 7, Picha: Brian Smith

Koffi aliongeza kuwa mashabiki wake watarajie shoo kali na yuko tayari kuwaburudisha watu anaowapenda nchini Kenya.