Millicent Omanga avunja kimya baada ya kuongoza orodha ya waliotafutwa Google 2023

Hata hivyo, wengine walimsuta na kumtupia vijembe vikali wakimwambia kwamba kumtafuta kwao katika mtandao huo si kwa manufaa mema bali walifanya hivyo kufuatia kashfa iliyosambaa mapema mwaka huu.

Muhtasari

• Omanga alikuwa wa kwanza kwenye orodha huku Dj Fatxo akikamata nafasi ya 3 akifuatiwa kwa karibu na Njenga katika nafasi ya nne.

Millicent Oamnga kuhusu suala la kitambi kwa wanawake
Millicent Oamnga kuhusu suala la kitambi kwa wanawake
Image: Facebook

Seneta maalum wa zamani Millicent Omanga hatimaye amevunja kimya baada ya Google kumtaja kuwa mkenya aliyetafutwa Zaidi katika mtandao huo katika mwaka wa 2023.

Omanga aliongoza orodha ya watu 10 humu nchini ambao Wakenya waliwatafuta Zaidi katika jukwaa la Google mwaka huu akifuatiwa na wengine ambao waligeuzwa gumzo Zaidi haswa nusu ya kwanza ya mwaka huu.

Omanga alijivunia kuongoza orodha hiyo na kupitia ukurasa wake wa Facebook ambao tayari umegonga Zaidi ya wafuasi milioni moja aliwashukuru mashabiki wake kwa kumwezesha kuwa Mkenya aliyetafutwa Zaidi Google 2023.

Hii mapenzi yangu na nyinyi nimekubali ni mia kwa mia . Nawalombotov Zaidi,” Omanga alisema.

Hata hivyo, wengine walimsuta na kumtupia vijembe vikali wakimwambia kwamba kumtafuta kwao katika mtandao huo si kwa manufaa mema bali walifanya hivyo kufuatia kashfa iliyosambaa mapema mwaka huu.

Itakumbukwa Omanga aligeuzwa gumzo la mitandaoni baada ya video ya utupu iliyodaiwa kuwa yake kuvujishwa.

Omanga alikuwa wa kwanza kwenye orodha huku Dj Fatxo akikamata nafasi ya 3 akifuatiwa kwa karibu na Njenga katika nafasi ya nne.

Omanga ni mwanasiasa mashuhuri wa Kenya, na Fatxo ni DJ wa Mugithi maarufu huku Njenga ni mwanamitindo maarufu wa Instagram aliyejipatia umaarufu baada ya uhusiano wake na Mchezaji nyota ”Baha” kutoka Machachari.

Watu hao watatu walikuwa na kitu sawa kwa kuona kwamba walivuma sana kwa sababu zisizo sahihi.

Mwanasiasa huyo alijipata kwenye jukwaa kuu la umaarufu baada ya video chafu iliyodaiwa kuwa yake, ikimuonyesha akiwa kitandani na kijana mdogo kuachiliwa.

Omanga hajawahi kuzungumzia suala hilo lakini alijibu kwa kuchapisha mstari wa Biblia siku chache baada ya video hiyo kuvuja mapema mwaka huu.