Mama Dangote asimulia safari ndefu amepita na mwanawe Diamond wakitafuta maisha

"Leo hii Sandrah Navaa saa ya dhahabu nijambo lakumshkuru Mwenyezi Mungu. Asante sana Mwanangu Naseeb,” alimaliza kwa shukrani.

Muhtasari

• "Sasa naombeni wamama wenzangu kuimba sio uhuni ni kazi kama kazi nyingine waacheni watoto wafanye au waonyeshe vipaji vyao, " Mama Dangote alisema.

Diamond na mamake
Diamond na mamake
Image: Instagram

Sandra, ama ukipenda Mama Dangote amesimulia kwa mapana safari ndefu ambayo amepitia na mwanawe Diamond Platnumz wakisaka unafuu wa maisha.

Mama Dangote alichapisha video akiingia kwenye chumba chake cha kifahari sebuleni na kandika aya ndefu kusimulia jinsi mwanawe amefanikisha kumbadilishia maisha hadi sasa naye anaonekana japo mtu mbele za watu.

Alisema kwamba alikuwa anazunguka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine akiwa na wanawe kumtafutia Diamond nafasi ya kuonesha kipaji chake katika matamasha ya kusaka vipaji, japo wengi kipindi hicho hawakumuelewa na walimtuhumu kwa kuzurura na watoto.

Nakama mimi ningekuwa nasikiliza maneno ya watu leo hii Mwanangu Naseeb kwasasa anafahamika @diamondplatnumz 🦁 kipaji chake kingepotea bure.. Kwakuwa nilikuwa naambiwa nawafundisha uhuni @_esmaplatnumz @romyjons hawa ndio nilikuwa nazurura nao juu yakuwa alikuwa anapenda sana mziki na mm ndio nilikuwa namba moja kumpeleka sehemu yoyote wanao saka vipaji sijali ata kukesha mpaka hasubuhi ili mradi mwanangu apate nafasi nae aimbe tu basi hapo roho yangu kwatu,” Mama Dangote alikumbuka kwa hisia.

Alisema kwamba watu wengi kipindi hicho walikuwa wanahusisha muziki na uhuni lakini yeye hakuweza kuwasikiliza na sasa hivi anavuna kutokana na kutowasikiliza walimwengu.

Kwa kumalizia, Mama Dangote alitoa wosia kwa wazazi wanaokandamiza vipaji vya Sanaa vya wanao, akisema kwamba kwake Diamond amefanikiwa kumbadilishia maisha kupitia kipaji cha muziki.

“Wazazi wenzangu nawasihi sana kama mtoto wako anakipaji chochote naomba muendeleze. Sasa naombeni wamama wenzangu kuimba sio uhuni ni kazi kama kazi nyingine waacheni watoto wafanye au waonyeshe vipaji vyao vina manufaa kwao na kwetu wazazi haya mm ningewasikiliza jee... Leo hii Sandrah Navaa saa ya dhahabu nijambo lakumshkuru Mwenyezi Mungu. Asante sana Mwanangu Naseeb,” alimaliza kwa shukrani.