Mpenzi wa Mungai Eve, atangaza azma lake kuu mwaka huu ni ku'adopt mtoto wa kiume

Ungamo la Trevor kuwa anatarajia kuadopt mtoto mwaka huu linafuata lile la awali mwaka jana ambapo alisema kwamba mipango yake na mpenziwe ni kupata mtoto wa kwao wa kumzaa angalau kuanzia 2026.

Muhtasari

• Zaidi ya maswali kuhusu familia yao inayozidi kupanuka, mashabiki pia wamekuwa na shauku ya kutaka kujua ni lini Trevor na Eve Mungai watafunga ndoa rasmi.

Director Trevor na Eve Mungai.
Director Trevor na Eve Mungai.
Image: Instagram

Director Trevor, mpenzi wa YouTuber Mungai Eve amezua minong’ono mitandaoni baada ya kudai kwamba moja ya malengo yake ya mwaka huu wa 2024 ni kuasili mtoto.

Trevor kupitia kipindi cha maswali na majibu katika Instagram alifichua hili wakati akimjibu shabiki mmoja ambaye alikuwa anamuuliza iwapo ana mtoto.

Trevor kwa ujasiri alisema kwamba hana mtoto ila angependa kuasili mtoto wa kiume mwaka huu.

"Nataka kuchukua mmoja. Mtoto wa kiume,” alisema.

Kidokezo hiki kinakuja wakati ambapo Trevor na Mungai Eve wamekuwa wakijipata chini ya shinikizo haswa suala la kupata mtoto linapotajwa au wao wanapoonekana wakitoa maoni yao kwa wenzao ambao wanatoa habari njema za kutarajia mtoto.

Itakumbukwa kwamba wawili hao ambao ndio YouTubers maarufu nchini wamekuwa pamoja kwa Zaidi ya miaka 5 lakini hawajawahi kuwa na mtoto licha ya hapo awali kuwepo kwa uvumi kuhusu Mungai Eve kuwa na ujauzito.

Ungamo la Trevor kuwa anatarajia kuadopt mtoto mwaka huu linafuata lile la awali mwaka jana ambapo alisema kwamba mipango yake na mpenziwe ni kupata mtoto wa kwao wa kumzaa angalau kuanzia 2026.

Zaidi ya maswali kuhusu familia yao inayozidi kupanuka, mashabiki pia wamekuwa na shauku ya kutaka kujua ni lini Trevor na Eve Mungai watafunga ndoa rasmi.

Katika kujibu maswali, Trevor alishukuru kwa udadisi na kushiriki:

"Ingawa hatuna tarehe mahususi ya arusi yetu bado, tunafurahia matarajio yetu ya wakati ujao pamoja na kushiriki mipango yetu wakati unahisi kuwa sawa kwa sisi sote."