Mungai Eve afuta picha za mpenziwe muda mfupi baada ya Trevor kudai anataka ku'adopt mtoto

Wawili hao wamedokeza mtafaruku katika penzi lao ikiwa ni saa chache baada ya Trevor kufichua kwa mashabiki wake kwamba anataka kuasili mtoto wa kiume, akionesha kukata tamaa kusubiri kuzaliwa wake.

Muhtasari

• Lakini je, unahisi kila mmoja kufuta picha za mwenzake ni ishara ya kuachana ama ni mbwembwe tu za kufukuzia kiki

Trevor na mpenzi wake Mungai Eve
Trevor na mpenzi wake Mungai Eve
Image: Instagram

Majasusi wa maisha ya watu maarufu mitandaoni wameanza mwaka 2024 kwa gia ya juu na habari mpya mitandaoni shukrani kwa juhudi zao ni kwamba kuna minong’ono ya kutokea kwa mfarakano katika huba la YouTuber Mungai Eve na mpenziwe Director Trevor.

 Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mitandaoni na ambazo zinaweza kuthibitshwa, Mungai Eve na Trevo, kila mmoja amefuta picha zote za mwenzake katika kurasa zao kwenye mtandao wa Instagram.

Hata hivyom haijulikani ni nini kilisababisha uamuzi huu wa ajabu kati ya wapenzi hao wa Zaidi ya miaka 5, lakini aghalabu wapenzi wanapochukua hatua ya kufuta picha za wenzao kwenye kurasa zao mitandaoni, huchukuliwa kama ishara ya penzi kuingia mchangani.

Lakini pia itakumbukwa hatua hii inajiri muda mfupi tu baada ya Director Trevor kufichua kwamba lengo lake kuu kwa mwaka huu 2024 ni ku’adopt mtoto, akisisitiza kwamba sharti mtoto huyo awe wa kiume.

Hili lilizua mjadala baadhi wakihisi kwamba huenda ameamua kufanya hivyo baada ya pengine Mungai Eve kuchelewesha kumzalia hali ya kuwa kijana wa watu ana nia ya dhati ya kuitwa baba kabla ya kulikunja jamvi la mwaka huu.

Awali Trevor ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa muwazi kabisa kuzungumzia masuala yake ya kibinafsi kwa mashabiki wake mitandaoni, alifichua kwamba watafunga ndoa na Mungai Eve na akasema mipango yao ipo kwamba watapata mtoto wao kuanzia mwaka 2026.

Lakini je, unahisi kila mmoja kufuta picha za mwenzake ni ishara ya kuachana ama ni mbwembwe tu za kufukuzia kiki?