Sababu ya Cassypool kuchukizwa na wanaochapisha picha za mimba na chakula mitandaoni

“Kuna watu ni tasa, wanalia usiku mzima, wanaambia Mungu awasaidie. Yeye ni shabiki wako halafu unampostia mimba. Unamwambia nini?” aliuliza.

Muhtasari

• “Kuna watu ni tasa, wanalia usiku mzima, wanaambia Mungu awasaidie. Yeye ni shabiki wako halafu unampostia mimba. Unamwambia nini?” aliuliza.

Cassypool
Cassypool
Image: Facebook

Mbwatukaji wa mitandaoni, Cassypool Capon ameanza mwaka 2024 akilenga vita dhidi ya watu maarufu ambao wanajipata mitandaoni kwa kuchapisha picha za vyakula na ujauzito katika mitandao ya kijamii.

Katika video ya hivi majuzi, Cassypool alisema kwamba kuchapisha picha za vyakula mitandaoni ni sawa na kumjaribu Mungu kwa kumuonesha kitambi cha shibe, jambo ambalo si sahihi kwani katika wafuasi wako mitandaoni, wengi wao huenda wanakumbwa na matatizo ya njaa hali ya kuwa wewe unajipiga kifua kuonyesha shibe.

“Umepost chakula ndio wafanye nini? Ni upuzi. Usikejeli na usionyeshe Mungu kitambi. Mungu akikubariki kwa chakula, kula. Stop posting. Do content. Kuna watu wanalala njaa,” Cassypool alisema.

 Vile vile, Cassypool aliwasuta wanaopakia picha za kuonesha ujauzito wao, akirejelea pale plae kwamba miongoni mwa wafuasi wao huenda kuna wengine wanatafuta mtoto bila mafanikio na wakiona ukionesha mimba wataitafsiri taswira hiyo kama unawakejeli na hivyo wewe utajipata kuwa sababu ya watu kujisikitikia bure bila wewe kujua.

“Kuna watu ni tasa, wanalia usiku mzima, wanaambia Mungu awasaidie. Yeye ni shabiki wako halafu unampostia mimba. Unamwambia nini?” aliuliza.