2Mbili aomba mashabiki kumchangia milioni 7 kununua gari kuadhimisha birthday yake

"“Tarehe 10 Januari ndio siku yangu ya kuzaliwa, BMW X4 ndio zawadi tu ambayo ninahitaji, na kwa kweli siwezi kumudu kuliminili ifikapo wiki kesho" 2Mbili aliomba.

Muhtasari

• Haya yanajiri siku mbili tu baada ya msanii Beka Flavour kutoka Tanzania kujitokeza mitandaoni pia akiomba kuchangishiwa pesa ili kumlipia mkewe mahari,

Mchekeshaji 2mbili na mwanamuziki Ngesh.
Mchekeshaji 2mbili na mwanamuziki Ngesh.
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji na YouTuber 2Mbili amewashanagza wengi baada ya kupeleka mitandaoni akiomba michango kutoka kwa mashabiki yake kwa ajili ya kufanikisha ndoto yake ya mwaka 2024 – kununua gari la kifahari aina ya BMW.

Mchekeshaji huyo kupitia kwa Instagram story yake, alichapisha picha ya gari hilo la samawati na kusema kwamba ndilo gari la ndoto zake lakini kwa bahati mbaya hawezi kupata kiasi cha pesa ambacho kinahitajika ili kulimiliki.

2Mbili alifichua kwamba gari hilo aina ya BMW X4 katika soko ya sasa linatoka kwa kima cha shilingi milioni 7 ambazo kwake ni mlima mrefu wa kuukwea hivyo kuomba mashabiki weney roho nzuri kumchangia kwa ajili ya kufanikisha ndoto yake kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa.

“Tarehe 10 Januari ndio siku yangu ya kuzaliwa, BMW X4 ndio zawadi tu ambayo ninahitaji, na kwa kweli siwezi kumudu kuliminili ifikapo wiki kesho, lakini kupitia kwa sapoti yenu ninaweza, ni shilingi milioni 7 tu,” 2Mbili aliandika na kumalizia na namba yake ya MPesa ambayo sisi hatuna kibali kuiweka hapa kwa sababu za kiitifaki.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya msanii Beka Flavour kutoka Tanzania kujitokeza mitandaoni pia akiomba kuchangishiwa pesa ili kumlipia mkewe mahari,

Beka katika mfululizo wa machapisho mitandaoni,c alisema kwamba mkewe alitoroka kwenda kwao na mwanawe na kujaribu kumfuata alikabiliana na masharti makali kutoka kwa wakwe.

Alisema kwamba wakwe zake walimtaka kulipa mahari ya kiasi cha milioni 22 za kitanzania ili kurudishiwa mkewe jambo Ambalo alisema asingeweza kumudu pasi na kusaidiwa.

Naye kama 2Mbili tu, alimalizia kwa kuchapisha namba yake akiomba kusaidiwa kumrudisha mkewe kwa kumlipia mahari.