Kwa nini dadake Pasta Kanyari aliharakishwa kuzikwa muda mfupi baada ya kuuawa?

Wengine pia walitilia shaka kuwa kuna kitu kilikuwa kinajaribu kufunikwa, kwani familia ya akina mchungaji Kanyari si ya misingi ya Kiislamu.

Muhtasari

• “Hiyo ni haraka sana, kwani wanajaribu kuficha nini tusichokijua?” Musau Eric.

 
• “Ni kama hawataki sifa mbaya lakini oops, wameshachelewa,” Wangui Macharia.

Starlet Wahu azikwa
Starlet Wahu azikwa
Image: Hisani

Jumamosi alfajiri Wakenya waliamkia taarifa za kushangaza kufuatia kuuawa kwa mwanasosholaiti Starlet Wahu ambaye ni dadake mchungaji Victor Kanyari.

Wahu aliripotiwa kupatikana ameuawa kinyama kwa kutumia kisu katika nyumba moja ya AirBnB mtaani South B na mwanamume ambaye waliripotiwa kuingia naye katika chumba hicho kufuatia picha za CCTV.

Hata hivyo, taarifa hizo zilichukua mkondo tofauti baada ya familia kuafikiana kumzika mrembo huyo mwenye umri wa miaka 24 hiyo hiyo Jumamosi, ikiwa ni saa chache tu baada ya kifo chake.

Tukio hili ambalo ni la kushangaza liliwashangaza watu wengi katika mtandao wa kijamii, wengi wakiibua maswali kuhusu ni kwa nini mazishi yake yaliharakishwa hivyo hata kabla ya uchunguzi kukamilika.

Wengine pia walitilia shaka kuwa kuna kitu kilikuwa kinajaribu kufunikwa, kwani familia ya akina mchungaji Kanyari si ya misingi ya Kiislamu – dini ambayo inajulikana kwa kufanya maziko kwa haraka hivyo.

Wahu aizikwa Jumamosi alasiri katika shamba la familia huko Kamulu kaunti ya Nairobi katika hafla ambayo ilihudhuriwa na watu wachache, wengi wao wakiwa wanafamilia tu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya Wakenya waliostaajabishwa na uharaka wa mazishi ya sosholaiti huyo kupitia mtandao wa X;

“Mimi nataka kuona jinsi eulogy iliandikwa tafadhali,” Benson Mwiti.

“Eei, hivyo tu, mii nimefikiri alifariki jana ama juzi,” Polo Kimanii.

“Hiyo ni haraka sana, kwani wanajaribu kuficha nini tusichokijua?” Musau Eric.

“Ni kama hawataki sifa mbaya lakini oops, wameshachelewa,” Wangui Macharia.

“Na ndivyo mazishi yanavyotakiwa kuwa! Matukio ya kibinafsi ya familia !!! Hazikusudiwi kuwa za umma au za fujo. Send off nzuri tu. Uungwana haufanani na ubadhirifu.” Ian Ogwa Ketenyi.

“Hii inapaswa kukufundisha tu kwamba maisha yanamaanisha kitu unapokuwa hai tu,” Duncan Kenya.