Edday Nderitu na wanawe waona theluji ya msimu wa baridi kwa mara ya kwanza USA

Edday aliondoka na wanawe Kenya mwaka jana na huu ndo umekuwa msimu wake wa kwanza wa baridi akiwa nchini Marekani.

Muhtasari

• “Watoto wangu hawangelisubiri kuona theluji, lakini wacha niwaambie baridi weh!” Edday aliandika kwenye picha hizo.

Edday Nderitu na wanawe
Edday Nderitu na wanawe
Image: Facebook

Kwa mara ya kwanza, mkewe Samidoh, Edday Nderitu na wanawe waona na kufurhia uzoefu wao kutembea kwenye theluji wakiwa nchini Marekani.

Nderitu ambaye alindoka nchini mwaka jana na wanawe wote katika kile kilichotajwa kuwa ni kuiasi ndoa yake na Samidoh alipakia picha katika ukurasa wake wa Facebook akiwa na wanawe 3.

Wanne hao walikuwa wamevalia mavazi ya kutia joto mwilini wakiwa wanatembea kwenye theluji nyeupe pe pe pe, ikiwa ni ndio mwanzo wa msimu wa baridi shadidi katika mataifa mengi ya Ulaya na Amerika.

Edday alisema kwamba ndio mara yake ya kwanza na wanawe kuona na kupitia msimu wa baridi na kusema kuwa baridi ambayo inakuwa katika majira hayo haina mfano wowote wa kuzungumziwa.

“Watoto wangu hawangelisubiri kuona theluji, lakini wacha niwaambie baridi weh!” Edday aliandika kwenye picha hizo.

Misimu ya joto na baridi aghalabu hushuhudiwa katika bara la Ulaya na Amerika lakini katika bara la Afrika na haswa katika mataifa yaliyo kaitka ukanda wa Equator misimu hiyo huwa haishuhudiwi.

Mama huyo wa watoto watatu majuzi pia ameonesha kukereka baada ya Samidoh kumpeleka babymama wake, Karen Nyamu katika nyumba ambayo walishirikiana kujenga na yeye kijijini mwao kaunti ya Nyandarua.

Edday katika hali ya kutaka kumpa Samidoh funzo, aliapa ya kwamba mumewe ataishia kuwaona wanawe katika mitandao ya kijamii tu wala hakuna muda atakaa na kuja kuonana nao ana kwa ana.