'Nitawawekea risiti ya bei ya chupi zangu' Zari awaambia wanaodai mavazi yake ni feki

“Sijisumbui hata na filter kwenye begi hili. Nimekuwa na begi hili kwa miaka mingi"

Muhtasari

•Alisisimka zaidi huku akiondoa risiti kutoka kwa begi lake la YSK ili kuonyesha jinsi Loius Vuitton ilivyomgharimu.

Zari Hassan
Image: Zari Hassan Instagram

Zari the Boss Lady ni mama mwenye mtindo wa kipekee wa maisha adimu ambayo anayaishi. Hii mara nyingi huwafanya wengi kuhisi kwamba wamefeli kimaisha na wengine hata kutaka kumchunguza juu ya mtindo wake wa maisha kitu ambacho kilitokea hivi majuzi.

Alishiriki picha na mkoba wa Louis Vuitton, akitembea kwa ustadi kuzunguka mbele ya baraza la nyumba yake ghali Afrika Kusini.

Mama huyo wa watoto watano alitembea kwa madaha kuelekea kwa gari lake la kifahari aina ya Jeep na kuingia ndani kwa mtindo wa kitajiri.

Alikuwa amevaa mavazi ya cream, yaliyounganishwa na mkoba.

Zari aliwapa usia mashabiki wake kwa kutumia kauli maarufu ya Dwayne Johnson akilenga kutuma ujumbe wa mtumaini kwamba mtu halali tu siku moja na kuamka akiwa tajiri bali utajiri ni jambo la hatua moja baada ya nyingine.

"Mafanikio hayaji mara moja. Ni wakati kila siku unakuwa bora zaidi kuliko siku iliyopita. Yote yanajumuisha." - Dwayne Johnson," alinukuu video ya Jumatatu Januari 8.

Mwanamume mmoja alimwambia kwa ujasiri kwamba mfuko wake ulikuwa bandia, na hii haikukaa vizuri naye.

Mama huyo wa watoto watano hakufurahishwa na ukosoaji huo na alijibu vikali akiandika hadithi zake kwenye Instagram ili kuwaelezea wakosoaji.

"Man f** it, what's 2k$," alianza kufoka.

zari
zari

Kuongeza;

“Naomba ukae kwenye broke lane yako acha kuandikia vitu vya watu feki, nitaweka risiti za nguo yangu ya ndani pia kwani nyinyi wote mnajifanya wanahusika sana.”

“Sijisumbui hata na filter kwenye begi hili. Nimekuwa na begi hili kwa miaka mingi na mwanamume mtu mzima anaropokwa 'Oh nimependa jinsi Zari anavyoendelea na maisha yake hafai...ameshika pochi feki, lakini hajali,'...kama nyie mnataka tuanze kuzunguka na mifuko feki?"

Alisisimka zaidi huku akiondoa risiti kutoka kwa begi lake la YSK ili kuonyesha jinsi Loius Vuitton ilivyomgharimu.