"Nimetabiriwa kufa 2028!" - Roma Mkatoliki, msanii wa rap ya Bongo

Kupitia ukurasa wake wa X, Roma alichapisha kwamba mtandao wa Google umtabiri kifo chake kitatokea Jumatano ya Januari 12 mwaka 2028.

Muhtasari

• “Unajua bei ya kusafirisha mwili kutoka state hadi hapa kwenye cargo?” Ninja Damour alimuuliza.

• "Wampe mama ivan hiyo hela wakishachanga, mm wanifukie hukuhuku,” alijibu Roma.

ROMA
ROMA
Image: FACEBOOK

Msanii wa rap za Bongo anayeimba tungo za kimapinduzi na kiharakati, Roma Mkatoliki amewashangaza mashabiki wake baada ya kudai kwamba ametabiriwa kifo chake kitatokea mwaka 2028.

Kupitia ukurasa wake wa X, Roma alichapisha kwamba mtandao wa Google umtabiri kifo chake kitatokea Jumatano ya Januari 12 mwaka 2028.

Aliwaingiza mjini mashabiki wake kuhusu huduma Fulani inayotabiri kifo cha mtu ambayo inapatikana kwenye Google kwa kutafuta maneno ‘Death Clock’.

Baada ya kutafuta maneno hayo, itakufungulia ukurasa mzima na kukuelekeza ubonyeze kwenye utabiri wa siku yako ya mwisho duniani – ‘Your Death Prediction Results’ ambayo itakupa majibu na matokeo ya siku yako ya mwisho.

Kwake baada ya kubonyeza hapo, alipigwa na butwaa kuambiwa kwamba ana chini ya miaka minne kuishi duniani.

“Ukienda Google Uka Search Pale Juu Ukaandika “DEATH CLOCK” Then Ukaingia Sehemu Imeandikwa "Matokeo ya Utabiri wa Kifo chako" Wanakupa Matokeo 😁😁😁. Mi Wamenambia 2028 Naamsha😁 Siku ya Mapinduzi Flani!! Khaaa!” Roma alisema.

Itakumbukwa miaka kadhaa iliyopita, Roma alitoroka Tanzania baada ya kudai kwamba maisha yake yalikuwa hatarini kwani alihisi kuwa alikuwa anawindwa na asasi za serikali kutokana na mwendelezo wa nyimbo zake za kiharakati ambazo zilikuwa zinalenga mabomu kwa serikali.

Kwa muda sasa, amekuwa akifanya shughuli zake za kisanaa akiwa nchini Marekani, na baadhi ya mashabiki wake walimtania kwamba anafaa kurudi ili akafie nyumbani ifikapo mwaka 2028.

Roma aliwajibu kwamba hela watakazochangisha kwa ajili ya kusafirisha mwili wake ni bora wakamuachie mama watoto wake, yeye yuko radhi kabisa kuzikwa Marekani, ishara kwamba hadi wakati amefariki, bado hajihisi kuwa salama kabisa kurudi Tanzania.

Unajua bei ya kusafirisha mwili kutoka state hadi hapa kwenye cargo?” Ninja Damour alimuuliza.

"Wampe mama ivan hiyo hela wakishachanga, mm wanifukie hukuhuku,” alijibu Roma.

 Kwa haraka, mtu yeyote akiangalia matokeo yake ya siku ya kufa kwenye mtandao huo, maotkeo mengi yanatoka mwaka 2028, kitu ambacho wengi wamekipuuzilia mbali kuwa ni mtandao wa hadaa.