Mwanamume 'mrembo' aonesha picha zake baada ya kufaulu upasuaji wa kubadili jinsia (Picha)

Bobrisky ambaye ni mwanamume aliyebadili jinsia yake kufuatia msururu wa upasuaji hivi majuzi alifanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti yake na kulainisha ngozi yake ya mwili.

Muhtasari

• Katika picha zilizotikisa hewani mtandaoni, Bobrisky akiwa amevalia mavazi meusi, alionekana akiwa amekaa vizuri kwenye kitanda chake, akionyesha sura yake mpya.

Bobriksy
Bobriksy
Image: Instagram

Crossdresser na sosholaiti wa Nigeria, Idris Okuneye anayejulikana zaidi kama Bobrisky amewasha taa za mchana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuibuka na picha mpya kuonesha jinsi amerembeka baada ya kufaulu katika upasuaji mwingine wa kuboresha urembo wake.

Bobrisky ambaye ni mwanamume aliyebadili jinsia yake kufuatia msururu wa upasuaji hivi majuzi alifanyiwa upasuaji wa kuongeza maziwa yake na kulainisha ngozi yake ya mwili.

Bobrisky, ambaye alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kukuza tezi ya matiti (Augmentation mammoplasty), alitumia ukurasa wake wa Instagram alipokuwa akishiriki baadhi ya picha zinazoonyesha umbo lake jipya la mwili.

Katika picha zilizotikisa hewani mtandaoni, Bobrisky akiwa amevalia mavazi meusi, alionekana akiwa amekaa vizuri kwenye kitanda chake, akionyesha sura yake mpya.

Bobrisky alinukuu, "Nzuri na ya kustarehesha, huo ni mtindo wangu."

Tazama picha zake hapa chini:

Bobriksy
Bobriksy
Bobrisky
Bobrisky
Bobrisky
Bobrisky

Wiki iliyopita tuliripoti kwamba mwanasosholaiti huyo aliyebadili jinsia alitoa ratecard yake ghali ikionyesha bei za baadhi ya huduma ambazo anapeana.

Katika orodha hiyo, Bobrisky alidai kwamba kwa mtu anayetaka kukutana naye kwa ajili ya salamu tu, ni sharti alipe kima cha shilingi laki tatu na ushee.