Vanessa Mdee atoa msimamo wake kuhusu ujio wa Akili Mnemba, maarufu kama AI

Msimako wake unakuja siku chache baada ya jarida la AFP kufichua kwamba wataalamu wa AI wanaendelea na mipango ya kufanya suala la kifo kuwa ‘si la lazima’.

Muhtasari

•Kwa Vanessa Mdee, hayuko tayari kuikumbatia akili mnemba kwa njia yoyote ile hata kama watu wanaomzunguka watamuita ‘mtu wa zamani’.

Vanessa Mdee
Image: Hisani

Malkia wa zamani wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ameweka wazi msimamo wake kuhusu ujio wa akili mnemba, maarufu kama AI.

AI ni akili bandia ambayo imewekwa kwa mashine za kufanya kazi na ina uwezo wa kufanya kazi na kufikiria kwa asilimia kubwa kama mwanadamu.

Ujio wa AI imekuwa ukizua tumbo joto miongoni mwa watu, haswa baada ya IMF kuonya wiki iliyopita kwamba AI itachukua asilimia 40 ya ajira ambazo kwa sasa zinatekelezwa kwa mikono ya binadamu.

Sasa Vanessa Mdee kupitia ukurasa wake wa Instagram ameota maoni yake kuhusu jinsi utandawazi huo mpya unavyokuja kwa kasi ya ajabu na kusukumwa na makampuni makubwa ya teknolojia yakiwemo Microsoft kupitia ChatGPPT, Google kupitia Bard lakini pia OpenAI.

Vanessa Mdee anatilia mashaka makubwa jinsi AI inavyosukumwa na kulazimishwa kwa watu kupitia huduma hizi za teknolojia ambazo zimeingiza utandawazi wa AI kwenye huduma zake.

Kwa Vanessa Mdee, hayuko tayari kuikumbatia akili mnemba kwa njia yoyote ile hata kama watu wanaomzunguka watamuita ‘mtu wa zamani’.

“Niite mtu wa teknolojia ya zamani lakini AI kwangu hapana kwa kweli, inanifanya nakuwa mwenye mashaka. Ni kwa jinsi inavyolazimishwa kwetu,” Vanessa Mdee alisema.

Mdee anatoa maoni haya siku chache baada ya jarida la AFP kufichua kwamba wataalamu wa AI wanaendelea na mipango ya kufanya suala la kifo kuwa ‘si la lazima’.

mdee
mdee