Nikipiga hesabu najiona mimi ni msanii namba 3 kwa hela Tanzania - Baba Levo

Msanii huyo alisema kwamba wasanii wengine ambao wamekuwa wakiogopwa kwa muda mrefu kumbe hawana kitu zaidi ya kukodisha vitu ili kujionyesha navyo mitandaoni.

Muhtasari

• Hata hivyo, Baba Levo hakuweza kumtaja msanii namba moja na namba mbili kwa pesa lakini inaonekana moja kwa moja katika hesabu zake alimpa bosi wake nambari moja.

Baba Levo
Baba Levo
Image: Instagram,

Msiri wa Diamond Platnumz, Baba Levo amefichua kwamba anahisi yeye ndiye tajiri namba tatu kwa watu walioko kwenye Sanaa nchini Tanzania.

Kupitia Instagram yake, Baba Levo aliandika kwamba amechanganua hisabati sana na kuibuka na jibu kwamba yeye ndiye anashikilia nafasi ya tatu kwa wasanii walio na hela nyingi.

Levo ambaye ni msanii na mtangazaji katika kituo cha redio cha Wasafi FM kinachomilikiwa na Diamond Platnumz alitambua kwamba hela nyingi ambazo sasa anajivunia kuwa nazoni kutokana na mchango wa bosi wake, Diamond.

“Mimi nikipiga hesabu najiona ni msanii namba tatu kwa hela Tanzania, hao wasanii wengine tulikuwa tunawaogopa hawana kitu, ni njaa tupu. Ahsante sana Lukuga [Diamond Platnumz]” Baba Levo alisema.

Baba Levo amekuwa chawa wa kumtetea na kumsifia Diamond Platnumz hadharani kwa kipindi cha miaka mingikiasi kwamba amefanya watu wengine wameanza kuhisi uchawa nao ni kazi ya kumuingizia mtu kipato mjini.

Hata hivyo, Baba Levo hakuweza kumtaja msanii namba moja na namba mbili kwa pesa lakini inaonekana moja kwa moja katika hesabu zake alimpa bosi wake nambari moja.

Wasanii wa Bongo Fleva kwa muda sasa wamekuwa kila mmoja alijishebedua na anachokimiliki cha thamani huku wakionyesha mitandaoni kwa mashabiki wao ili kutamba.