Baba Levo asherehekea, mwanawe wa mwezi mmoja apata dili nono

Diamond na mpeziwe Zuchu wakipata mtoto nitawazawadi Nepi Baba Levo asema

Muhtasari

•"Nina furaha sana mtoto wangu wa mwezi mmoja  'P Platinumz' ambaye ni mjukuu wa Diamond kuchanguliwa rasmi  na picha yake kutumika kama balozi,"Baba Levo.

Baba Levo
Baba Levo
Image: Screengrab

Mwimbaji wa Bongo mkongwe Baba Levo alikuwa mwenye furaha baada ya mtoto wake wa mwezi  mmoja  kuchanguliwa na kampuni moja ya Nepi kama balozi wa maunzo kwa muda wa miaka mitatu.

Chawa huyo wa WCB alikuwa mwingi wa furaha huku akifunguka kuwa ni Maombi yake Bosi wake Diamond Platnumz pamoja na aliyemtaja kuwa mpenziwe Zuchu wabarikiwe na mtoto ili awe wa kwanza kumpa zawadi za Nepi zenye chapa za mtoto wake.

Baba Levo amemtwika mwanawe jina 'Mjukuu wa Diamond' kwani yeye husema licha ya kumzidi umri Diamond yeye tu ndiye babake kwa kumlea kimziki. 

"Nina furaha sana mtoto wangu wa mwezi mmoja  'P Platinumz' ambaye ni mjukuu wa Diamond kuchanguliwa kwa umri wa mwezi mmoja na picha yake rasmi kuchapishwa kama balozi wa mauzo katika kampuni  nashukuru sana mtoto mdogo kama huyo kuanza kupokea hela kwenye utoto wake,"alisema Baba Levo.

Baba Levo kwenye mahojiano alisimulia kuwa aliamua kumuita mtoto wake P Platinumz kwani kulingana naye Diamond ndiye Babu yake na ipo siku atamtembelea mjukuu wake na kumvalisha Nepi hizo.