"Alikiba ni muimbaji na Diamond ni mburudishaji," Master Jay aukata mzizi wa fitina

“A-list ya wasanii wetu wote sijui Diamond, Harmonize, Marioo ni best entertainers lakini sio waimbaji bora,” alisema. “Muimbaji bora ni Alikiba,” aliongeza.

Muhtasari

• Alisema kwamba tofauti kubwa kati ya Diamond na Alikiba ni kwamba mmoja ni mburudishaji bora na mwingine ni muimbaji bora.

Alikiba amtupia bomu la moto Diamond kisa wimbo wa kura
Alikiba amtupia bomu la moto Diamond kisa wimbo wa kura
Image: FACEBOOK, INSTAGRAM

Jaji wa Bongo Star Search na mzalishaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Master Jay ameamua kuukata mzizi wa fitina ambao umekuwa ukishikiliwa baina ya mashabiki wa wasanii wawili wakubwa wa Bongo Fleva – Diamond Platnumz na Alikiba.

Akizungumza katika mahojiano kwenye stesheni ya East Africa, Master Jay alisema ni wakati sasa mashabiki wang’amue kwamba kuna tofauti kubwa baina ya wasanii hao wawili na hakuna la kuwashindanisha nalo.

Alisema kwamba tofauti kubwa kati ya Diamond na Alikiba ni kwamba mmoja ni mburudishaji bora na mwingine ni muimbaji bora.

Alimtaja Alikiba kama mfalme katika kutunga na kuimba tungo nzuri kwa sauti ya kutamanisha huku akisema kwamba Diamond ni mzuri katika vimbwanga vya kutumbuiza haswa kwenye majukwaa.

Alikiba ni muimbaji bora na Diamond ni mburudishaji bora. Watu wabishe vile wanataka ila mimi ndio nimeongea kwenye Mic kabisa. Kuna kuimba na ku-entertain na kwenye muziki lazima ujue kuimba na ku-entertain,” Master Jay alisema.

Mkongwe huyo katika tasnia ya Bongo Fleva ambaye amewahi zungumziwa kwa njia mbalimbali kwa kumkandamiza Harmonize kwenye BSS kuwa hajui kuimba aliwataja baadhi ya wasanii wanaofanya vizuri katika Bongo Fleva na kusema kwamba wengi wao ni waburudishaji tu wala si waimbaji.

“A-list ya wasanii wetu wote sijui Diamond, Harmonize, Marioo ni best entertainers lakini sio waimbaji bora,” alisema. “Muimbaji bora ni Alikiba,” aliongeza.

Alisema kwamba kinachokwamisha Bongo Fleva kutusua kimataifa ni Wabongo kukosa kuwa na utambulisho wao wa kipekee na badala yake wanaparamia kuiga beat za watu kutoka Afrika Magharibi na Kusini.

“Tukitaka kwenda International lazima uwe na Identity yako, huwezi kuona Davido, Asake au msanii wa South Africa wanafanya sound ya BongoFleva. Kwa hapa East Africa wasanii wetu(Tanzania) ni bora na wanatengeneza pesa lakini hawatafika soko la kimataifa.”