Harmonize akiri kuwa nyuma ya popo wa 'kichawi' aliyening'inia mlangoni mwa Diamond

Harmonize aisema kwamba kuanzia sasa atakuwa anamtuma popo wake kwa watu na mtu yeyote anayetokewa na popo bila kusema kwa umma basi ataendelea kusumbuliwa na popo mpaka aseme.

Muhtasari

• Alimtania Diamond kwamba uzuri yeye aliweza kusema na kuweka hadharani kwa mashabiki wake kwa hiyo zamu ya kutembelewa na popo tena basi.

Harmonize akiri kumtuma popo kwa Diamond
Harmonize akiri kumtuma popo kwa Diamond
Image: Instagram

Msanii Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram amewashangaza mashabiki wa Bongo Fleva baada ya kuonekana kukiri kuwa nyuma ya popo ambaye Diamond alimpata amening[inia katika mlango wake wa kuingilia ndani.

Jumanne Diamond alionesha wasiwasi na mashaka makubwa baada ya kurudi nyumbani kutoka katika maandalizi ya mwisho ya kuachia video yake ya Mapoz akiwashirikisha Jay Melody na Mr Blue na kumkuta mnyama popo amening’inia katika mlango wake.

Hiyo ni baada ya kutangaza awali kwamba alitarajia kuachia video yake Jumatano saa nne asubuhi lakini kutokana na kumkuta popo huyo ambaye alidai ni wa kichawi ambaye ametumwa na washindani wake katika muziki ili kuzuia nyota ya video yake kutotamba, alichelewesha kuachiliwa kwa video hiyo kwa hadi saa mbili.

Sasa Harmonize mwenyewe ameonekana kukiri kuwa nyuma ya yule popo aliyemtisha Diamond na kusema kwamba kwa sasa yeyote anayemtilia shaka anaweza kumuita ‘Mzee Popo’.

Harmonize katika video akiwa ofisini kwake alikuwa akicheka na washikaji wake na kusema kwamba kuanzia sasa atakuwa anamtuma popo wake kwa watu na mtu yeyote anayetokewa na popo bila kusema kwa umma basi ataendelea kusumbuliwa na popo mpaka aseme.

Alimtania Diamond kwamba uzuri yeye aliweza kusema na kuweka hadharani kwa mashabiki wake kwa hiyo zamu ya kutembelewa na popo tena basi.

“Ukipenda niite mzee popo. Popo bawa. Nikikujia usipotangaza anarudi. Bora umesema ndugu yangu. Naitwa Mzee Popo,” Harmonize alisema.

Diamond alikuwa ameingiwa na wasiwasi mkubwa akisema kwamba popo huyo alikuwa ni wa kichawi ambaye alitumwa kumwinda.

Baada ya wasiwasi mwingi, mmoja wa marafiki zake alichukua kijiti kirefu na kumng’oa yule popo mlangoni pa Diamond kabla ya kuweza kuingia.