Diamond Platnumz ahisi kutumiwa uchawi nyumbani kwake popo akining'inia mlangoni

Diamond kwa sauti ya wasiwasi alisema kwamba popo huyo si wa kawaida bali ni wa kutumwa na wachawi haswa baada ya kutangaza kuachia video yake mpya mwendo wa saa nne asubuhi ya Jumatano.

Muhtasari

• Kwa kawaida, wabongo wanaamini sana katika uwepo wa uchawi na nguvu za kishirikina katika baadhi ya vitu na matukio.

Diamond atumiwa popo
Diamond atumiwa popo
Image: Screengrab

Msanii anayetajwa kama mburudishaji bora kutoka Tanzania, Diamond Platnumz ameonesha kushtushwa kwake baada ya kurudi nyumbani na kumkuta popo kaning’inia katika mlango wa nyumba yake.

Msanii huyo alichapisha video hiyo kwenye insta story yake na kuonesha wasiwasi akisema kwamba pengine ametumiwa mkosi au uchawi katika nyumba yake kwa njia ya popo.

Kwa Maelezo ya Diamond amesema hakuwa popo wa kawaida Ni wakichawi hivyo ametumwa kwasababu Alitangaza kuachia Video ya Nyimbo yake Mpya Leo saa 10:00 am Asubuhi.

“Jamani, nimefika hapa, nakutana na popo eti, jamani inabidi sasa hiyo video tusitoe kesho,” alisikika akisema kwa sauti iliyojaa wasiwasi.

Hapo hapo mmoja wa watu wake alichukua mkwaju mrefu na kujaribu kumuondoa popo yule huku wenzake wakimtahadharisha kuwa makini kwani popo mwenyewe kwa maelezo yao hakuwa popo wa kawaida kabisa.

Kwa kutumia mkongojo ule, jamaa huyo aliweza kufanikisha kumuondoa popo yule kwenye kizingiti cha mlango huku Diamond na wenzake wakichanganyikiwa na nusura kutoroka popo akiwachanganya.

Kwa kawaida, wabongo wanaamini sana katika uwepo wa uchawi na nguvu za kishirikina katika baadhi ya vitu na matukio.

Hii ndio sababu kubwa kwa nini idadi kubwa ya waganga wa jadi bado wamo katika shughuli zao kwa wingi nchini humo, Waswahili hao wakiamini kwamba katika kila jambo baya linalowatokea kuna mkono wa mtu, kwa hiyo suluhu ni kwa mganga wa jadi.

Hata hivyo, taasisi za kisheria na serikali kwa muda mrefu zimekuwa zikisisitiza kwamba suala la uchawi ni la kufikirika tu wala halipo kwani ni vigumu kwa mtu kutoa uthibitisho tosha wa kushawishi mahakama kuhusu uchawi.