Diamond kuacha muziki na kurudi kijijini kufanya ukulima kisa ubishi wa Harmonize

Diamond anahisi hatua ya Harmonize kuendelea kubisha kuwa wimbo wake wa Single Again ndio mkubwa kwa mwaka 2023 kuliko ule wa Enjoy ni sawa na kuapizwa.

Muhtasari

• Msanii huyo mpenzi wa zamani wa Vanessa Mdee hakuishia hapo, alikwenda mbele na kutoa takwimu zote katika majukwaa mbalimbali.

Diamond na Harmonize
Diamond na Harmonize
Image: Facebook

Bosi wa lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz ameweka wazi hisia zake kuhusu kuacha masuala ya muziki iwapo wapinzani wake wataendelea kuzua ubishi kwamba ngoma zao zinauzidi wimbo wake na Juma Jux – Enjoy.

Diamond alidhihirisha wazi wazo hili kupitia ukurasa wa Instagram pale msanii Juma Jux alipopakia kipande cha wimbo huo na kutoa takwimu za jinsi umekuwa ukifanya kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali ya kupakua miziki.

Kwa mujibu wa Juma Jux, wimbo wa Enjoy ambao una miezi mitano tu kwenye masoko umefanya vizuri na ndio unasalia wimbo wa pekee kutoka Afrika Mashariki kupata takwimu za juu katika mwaka 2023.

Enjoy ni wimbo wenye miezi 5 tu, Lakini streams zake 🥶🤦🏽️ na matokeo yake ni makubwa kuzidi wimbo wowote ulitoka 2023 in East & Central Africa. Wimbo unao ongoza kupendwa na kila rika yani wazee, vijana hadi watoto. Umaarufu wa wimbo huu unadhihirika katika matukio na mazingira mbali mbali tuliyoshuhudia ya watu binafsi hadi ya kiserikali.”

“Naweza sema umaarufu wake huufanya kuwa wimbo unaoleta unit kwenye mataifa yetu ya East & Central Africa. Maana ukiona video clip ya nchi yoyote hapo unaweza kudhani ni clip ya Tanzania. 🥺️ It’s an endless love kuona mataifa mbali mbali yakikumbatia furaha inayoletwa na wimbo huu katika maisha yao.” “Kwa ufupi haipingiki “Enjoy” ni wimbo bora wa 2023. Me & My brothers @diamondplatnumz & @s2kizzy tunawashukuru wote mlioufanya huu wimbo kuwa wakipekee kwa njia yoyote. Tunawapenda sana 🙏🏾❤✌🏾” Jux alisema.

Msanii huyo mpenzi wa zamani wa Vanessa Mdee hakuishia hapo, alikwenda mbele na kutoa takwimu zote katika majukwaa mbalimbali.

Diamond alifika kwenye ukurasa huo na kuweka wazi kwamba amchoka kuwasikia wapinzani wake kimuziki kuendelea kutamba kwamba ngoma zao ndizo zilifanya vizuri mwaka 2023.

Kutokana na hilo, Diamond alisema kwamba endapo wataendelea hivyo basi yuko tayari kuachia muziki na kurudi kijijini mwao Kigoma – magharibi mwa Tanzania ili kujishughulisha na ukulima wa mawese.

“Wakiweka Ngoma Yoyote ya Mwaka jana yenye Rocords hizo ndani ya Miezi Michache hio, Mie Naacha Mziki naenda Kigoma Kulima Mawese huku naskiliza Nyimbo yangu ya Mwisho MAPOZ!” Diamond alisema.

Bila shaka hapa alionekana kumpiga mkwara mpinzani wake Harmonize ambaye amekuwa akijipiga kifua kwamba wimbo wake wa Single Again ndio wimbo pekee kutoka Bongo uliofanya vizuri kwa mwaka 2023.