Alikiba aungana na Nandy kumdondosha Diamond na matikiti yake kutoka 'trending'

Alikiba alimchamba Diamond kwa kutumia mstari wake kwenye wimbo wake wa Mapoz anapzungumzia kuhusu ‘matikiti kuangushwa’.

Muhtasari

• Hili bila shaka lilionekana kuwa tamko la kumkejeli Diamond ambaye katika wimbo wake wa Mapoz aliimba;

•“Matikiti kudondoka, Matikiti kudondokea.”

Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba ameamua kuendeleza vita vyake vya maneno na mtani wake wa tangu jadi, Diamond Platnumz baada ya wimbo wake mpya kupiku wimbo wa Diamond katika kushikilia nafasi ya kwanza kwenye ‘trending’.

Itakumbukwa wiki moja iliyopita, Diamond aliachia wimbo wake akimshirikisha Mr Blue na Jay Melody kwa jina Mapoz.

Wimbo huo ulikuja kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba ulishikilia nafasi ya kwanza kwa nchini Tanzania kwenye trends, lakini haukuweza kukaa sana kwani Alikiba naye alishirikiana na Nandy na kuachia wimbo kolabo yao kwa jina Dah!

Wimbo wa Nandy na ALikiba uliutengwa ule wa Mapoz wa Diamond kutoka nafasi ya kwanza kwenye trends nchini Tanzania na hili halikumuacha salama Diamond kwani Alikiba alichukua fursa ya kumpiga kumbo kwenye kitovu.

Kupitia Instastory yake, Alikiba alipakia picha ya jinsi wimbo wake na Nandy ‘Dah!’ umepata mapokezi katika nchi tofauti tofauti, ukiwa nambari moja nchini Tanzania, nambari 5 Kenya miongoni mwa mataifa mengine.

Alikiba alimchamba Diamond kwa kutumia mstari wake kwenye wimbo wake wa Mapoz anapzungumzia kuhusu ‘matikiti kuangushwa’.

Aliandika Alikiba;

“Dah! On trending. Go Nandy, umeangusha matikiti ya watu.”

alikiba
alikiba

Hili bila shaka lilionekana kuwa tamko la kumkejeli Diamond ambaye katika wimbo wake wa Mapoz aliimba;

Matikiti kudondoka, Matikiti kudondokea.”

Utani wa wawili hao umekuwa ukiendelea kwa muda lakini juzi produsa mkongwe wa Bongo Fleva, Master Jay aliwataka mashabiki kuacha kuwalinganisha akisema kwamba hawafanani kisanaa.

Jay aliweka wazi na sababu juu kwamba Alikiba ni muimbaji bora huku Diamond akiwa kama mburudishaji bora kwa hivyo haifai watu kuendelea kuwalingalisha kwa kitu chochote kile.