Diamond hawezi kunichukia kisa nimecheza wimbo wa msanii wa Alikiba - DJ Romy Jones

Mcheza santuri huyo alisema kwamba hawezi kuzuia kucheza wimbo mkali kisa ni wa msanii kutoka kwa lebo pinzani," alisema.

Muhtasari

• Tukio la hivi punde ambalo lilizua tumbojoto naina ya mashabiki ni baada ya Jons kucheza wimbo wa msanii Vanilla, ambaye yuko chini ya lebo ya Alikiba, Kings Music.

RJ THE DJ
RJ THE DJ
Image: INSTAGRAM//ROMY_JONS

Naibu msimamizi wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi ambaye pia ndiye mcheza santuri rasmi wa Diamond Platnumz, Romy Jons ametetea hatua yake ya kucheza nyimbo za wasanii wa lebo pinzani.

DJ huyo ambaye pia ni kakake Diamond Platnumz alihojiwa katika kituo kimoja ambapo aliulizwa kuhusu kucheza ngoma za wasanii kama vile Harmonize na Alikiba, licha ya kujua fika kwamba wawili hao ni mahasimu na bosi wake Diamond.

Tukio la hivi punde ambalo lilizua tumbojoto naina ya mashabiki ni baada ya Jons kucheza wimbo wa msanii Vanilla, ambaye yuko chini ya lebo ya Alikiba, Kings Music.

 Kwa kujitetea, Jons alisema kwamba hakuwa anajua kama Vanilla ni msanii chini ya lebo ya Alikiba lakini pia akasema kwamab bosi wake [Diamond] hawezi kumchukia kwa kufanya hivyo.

Mcheza santuri huyo alisema kwamba hawezi kuzuia kucheza wimbo mkali kisa ni wa msanii kutoka kwa lebo pinzani, kwani kama wasanii wa Bongo wanataka tasnia yao iende mbali basi ni sharti wakumbatie ushirikiano kutoka ngazi za kinyumbani ndio watusue kimataifa.

"Vanilla ana kipaji anaimba vizuri halafu mimi sijawahi jua kama yupo kwa Alikiba au wapi mimi naona tu anaimba vizuri basi, Halafu sisi tupo wachache sana kama tukisema tushirikiane tunaweza kufika mbali maana njee hatupo kabisa," alisema.

RJ the DJ, kama anavyojiita kisanaa alijitetea Zaidi akisema kwamba siku za nyuma aliwahi cheza wimbo wa Harmonize, Single Again na hivyo ndivyo inatakikana kupaishana kukiwepo na nafasi kwa lengo chanya katika tasnia ya Bongo Flava.