Machozi ya Ex wangu yaliniachia laana, siendelei - Lukamba, aliyekuwa mpiga picha wa Diamond

“Nimekuwa siendelei na hata mahusiano yangu hayadumu, nahisi kabisa kuna namna laana inanitafuna Kwa maumivu niliyompatia ambayo yalimfanya amwage machozi," alimaliza kwa sauti ya majuto.

Muhtasari

• Msanii huyo hata hivyo alijikung’uta mavumbi akijipa moyo kwamba si yeye alikuwa mwenye makosa kipindi wanaachana bali pia mpenzi wake alikuwa anamkosea.

Msanii Lukamba akizungumzia madhira aliyopitia Wasafi
Msanii Lukamba akizungumzia madhira aliyopitia Wasafi
Image: Instagram

Mpiga picha wa zamani wa msanii Diamond Platnumz ambaye pia kwa sasa ni msanii wa kujisimamia, Lukamba amefichua kwamba anahisi mkwamo wake kimaisha umesababishwa na mpenzi wake wa zamani.

Katika mahojiano ya hivi majuzi, Lukamba alisema kwamba kipindi wanakorofishana mpaka kuachana na mpenzi wake wa kwanza kwa jina Shuu Mimi, mrembo huyo aliondoka kwa njia ya kishari kiasi kwamba alitiririkwa na machozi.

Lukamba sasa anahisi maisha yake kutoenda jinsi alivyokuwa akitarajia kipindi anaondoka Wasafi huenda ni kutokana na machozi na mpenzi huyo wake wa kwanza.

Lukamba alisema kwamba anahisi kabisa machozi ya Shuu Mimi hayakumuacha salama kwani huenda yalikuwa ni machozi ya laana.

Kuna namna nahisi machozi ya mke wangu wa kwanza (Shuu Mimi) hayakwenda bure kuna laana yameniachia kutokana na nilichomtendea,” Lukamba alisema.

Msanii huyo hata hivyo alijikung’uta mavumbi akijipa moyo kwamba si yeye alikuwa mwenye makosa kipindi wanaachana bali pia mpenzi wake alikuwa anamkosea.

Alifichua kwamba kinachomfanya kuhisi machozi yake yalimuacha na laana ni kwa sababu kipindi anaanza maisha bila kuwa na kitu chochote cha thamani, Shuu Mimi alikwama naye lakini baada ya kupata vya kumiliki, wakaanza kukorofishana hadi kuachana hatimaye.

“Sio kwamba mimi ndio nilikuwa na makosa kiasi hichooo, hapana, hata yeye alikuwa anakosea, ila yeye ndiye mwanamke ambaye wakati naanza naye mahusiano sikuwa na kitu lakini alinivumilia, alikuwa ananisaidia nikikwama na zaidi alikubali kunizalia lakini nilikuja kumuacha kwa njia ambayo hakustahili kuachwa vile," Lukamba alifichua kwa majungu.

Kutokana na mazingira ya kijeuri ambayo Lukamba alimuacha mke wake wa kwanza, sasa anahisi machozi yake yamesababisha hata mahusiano yake mengine huwa hayana tija na hata kazi zake za Sanaa haziendi kabisa.

“Nimekuwa siendelei na hata mahusiano yangu hayadumu, nahisi kabisa kuna namna laana inanitafuna Kwa maumivu niliyompatia ambayo yalimfanya amwage machozi," alimaliza kwa sauti ya majuto.

Luka,ba aliondoka Wasafi mwaka 2022 na kusema anaanzisha chapa yake mwenyewe. Mwanzoni aliachia ngoma kiasi lakini hazikuwahi kutusua kama ambavyo wengi walikuwa wanatarajia.