Robert Alai ataja sababu anahisi Mungai Eve anastahili kumchukulia Trevor hatua za kisheria

Hii ni baada ya Trevor Jumatatu kufunguka kwamba amempiga kalamu Mungai Eve kutokana na kujihusisha na akaunti hizo.

Muhtasari

• Trevor alisema kwamba huduma za Mungai Eve hazihitajiki tena katika akaunti hizo na kwenda mbele na kutangaza kwamba amezibadilisha akaunti hizo majina mara moja.

Image: INSTAGRAM// MUNGAI EVE

MCA wa Kileleshwa ambaye pia ni mwanablogu Robert Alai amemrai YouTuber Eve Mungai kutotebwereka tu na kuangalia aliyekuwa mpenzi wake Director Trevor akiponyoka na akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zilikuwa za kikoa baina yao.

Kupitia ukurasa wake wa X, Alai alimshauri Mungai Eve kutathmini kupiga hatua nyingine ya mahakamani kutafuta haki.

Alai alisema kwamba Mungai Eve ndiye alitoa mchango mkubwa katika ukuaji wa chaneli zao za mitandao ya kijamii ambapo walikuwa wanajipatia riziki kipindi wako pamoja kama wapenzi.

“Hata Mungai anapaswa kumshtaki Trevor na kurejesha akaunti zake zote. Eve Mungai alitengeneza akaunti hizo kwa kutumia taswira yake na akaenda kuweka kila kitu ili akaunti hizo zikue. Nakumbuka ni mara ngapi tulitangamana naye tukifuatilia hadithi. Hapaswi kuruhusu chaneli kwenda kwa urahisi hivyo,” Robert Alai alishauri.

Hii ni baada ya Trevor Jumatatu kufunguka kwamba amempiga kalamu Mungai Eve kutokana na kujihusisha na akaunti hizo.

Trevor alisema kwamba huduma za Mungai Eve hazihitajiki tena katika akaunti hizo na kwenda mbele na kutangaza kwamba amezibadilisha akaunti hizo majina mara moja.

Kubadilisha akaunti hizo majina kunakuja wiki kadhaa baada ya wawili hao ambao walikuwa wakichumbiana kwa Zaidi ya miaka 6 kudaiwa kuachana katika hali isiyojulikana.

Baada ya kubadilisha chaneli hizo majina, kumekuwa na maoni mbali mbali mitandaoni, huku kukiibuka makundi mawili – moja la kumtetea Mungai na lingine la kumtetea Trevor kutokana na hatua hiyo mpya.

Hata hivyo, Mungai Eve hajazungumza chochote kwani kwa sasa yuko Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kujivinjari.