Wanandoa wengi hawafurahishani kwa tendo la ndoa, wanabakana tu - Pasta Mgogo (video)

“Kuna watu ambao wanasema eti tendo la ndoa sio lazima, sio chakua, eti ni kitu cha ziada… wewe usijidanganye, hiyo nayo ni meza ya Bwana, inapaswa kuliwa kwa maandalizi muhimu." alisema.

Muhtasari

• Aliwataka wanaume kuwa wapole katika suala la ndoa kwani mwanamke anachukua muda kupata hisia za kufanya mapenzi tofauti na wanaume.

Pasta Daniel Mgogo
Pasta Daniel Mgogo
Image: Facebook

Mchungaji maarufu kutoka Tanzania, Daniel Mgogo amedai kwamba watu wengi walioko katika ndoa hawafurahii tendo la ndoa bali wanaishi kwa kubakana tu.

Katika mahubiri ambayo video yake aliipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, Pasta Mgogo alisema kwamba watu wengi katika ndoa wanalichukulia suala la kujamiiana kimzaha hali ya kuwa ndilo suala kuu katika uhusiano wowote baina ya mke na mume.

“Kuna watu ambao wanasema eti tendo la ndoa sio lazima, sio chakua, eti ni kitu cha ziada… wewe usijidanganye, hiyo nayo ni meza ya Bwana, inapaswa kuliwa kwa maandalizi muhimu. Wanandoa wengi hamna hata maandalizi ya hiyo, mnaparamiana tu,” Mgogo alihubiri.

“…ubakaji unaoendelea ndani ya ndoa ni hatari. Na ndio maana kina mama wengi mko hapa hamwezi kusema, lakini ukweli hamfurahii tendon a ndoa na wanaume wenu. Kwa sababu halina maandalizi,” aliongeza.

Mchungaji huyo alisema kwamba waathirika wengi katika ndoa ni wanawake na kuwataka wanaume kuwa wapole katika suala la ndoa kwani mwanamke anachukua muda kupata hisia za kufanya mapenzi tofauti na wanaume.

“Mnawaumiza tu wake zenu, ni vile tu hawawezi kusema. Wananiambia mchungaji unaposimama kufundisha waambie, wanatubaka hawatuandai. Washa kwanza mama aanze kuongea lugha ya Kigiriki ndio uingie. Haraka ya nini wanaume?” Mgogo aliuliza.