Burna Boy, 32, afichua sababu kuu kwa nini hajawahi fikiria kufunga ndoa (video)

Kulingana na msanii huyo anayejiita Odogwu, anamwamini Mungu kumpa mke wa ‘kufanya akili’.

Muhtasari

• Video hiyo ilizua hisia nyingi huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakishiriki mawazo yao kupitia sehemu ya maoni.

Burna Boy
Burna Boy
Image: Facebook

Mwimbaji wa Nigeria aliyeshinda tuzo, Damini Ebunoluwa Ogulu, almaarufu Burna Boy, amefichua kwa nini bado hana haraka ya kuingia katika ndoa licha ya kuwa na ufanisi mkubwa kimaisha.

Katika video yake ya siku za nyuma ambayo imeibuliwa mitandaoni, Burna Boy alikuwa anazungumza na mashabiki wake moja kwa moja wakati mmoja alimuuliza sababu yake ya kutokuwa na mke licha ya umri wake kuzidi kwenda.

Burna Boy, anayetambuliwa kwa uchezaji wake wa hivi majuzi katika usiku wa tuzo ya Grammy ya 2024, alidai kuwa bado hajapata mwanamke sahihi, ambayo inachelewesha ndoa yake akiwa na umri wa miaka 32.

Kulingana na msanii huyo anayejiita Odogwu, anamwamini Mungu kumpa mke wa ‘kufanya akili’.

Mvunja rekodi ya ‘Last Last’ alizidi kusema kwamba anachukia wakati wanawake wanajaribu kutumia uwongo na ajenda za uwongo ili tu kuwa naye kimapenzi.

Kwa maneno yake, “Mungu akisema nioe, nitaoa. Mungu ndiye anayefanya yote, mimi ninafuata tu. Simchukii mtu yeyote, sipendi walipotumia uwongo na ajenda.”

Video hiyo ilizua hisia nyingi huku watumiaji wa mitandao ya kijamii wakishiriki mawazo yao kupitia sehemu ya maoni.

Itakumbukwa msanii huyo ambaye mara nyingi anachukiwa na mashabiki wa kike kwa kumpa mamake asilimia kubwa ya kuongoza na kuendesha maisha yake uhusiano wake wa mwisho ambao ulijulikana alikuwa na msanii wa Uingereza, Stefflon Don.

Baada ya kuachana, Don alifanya mahojiano mbalimbali ya kumchafua Burna Boy akisema kwamba anamsikiliza mama yake Zaidi kuliko mpenzi wake na pia ikadaiwa kwamba Don aliwahi sema Burna Boy hana uwezo wa kumzalisha mwanamke.