Hamisa achochea moto wa gumzo kuhusu nani baba kwa mwanawe mwenye historia tata

Baadhi walihisi muonekano mpya wa Dylan moja kwa moja anamfanana Latiffa, binti wa Diamond na Zari na kuhoji kwa nini hatambuliki kama wake.

Muhtasari

• Lakini safari hii, wengi walisema kwamba picha mpya ya mtoto huyo inaonyesha chembechembe za Diamond kwa mbali .

Dylan
Dylan
Image: Instagram

Kwa mara ya kwanza aliposherehekea mwanawe siku yake ya kuzaliwa miezi minne iliyopita, Hamisa Mobetto amechapisha picha ya mwanawe Dylan tena.

Mjasiriamali huyo alikuwa katika ziara ya kujivinjari na mwanawe nchini UAE ambapo alipakia picha yake na kama kawaida, hili liliibua minong’ono ambayo imekuwa ikienezwa kwa muda mrefu pasi kuwepo na jibu.

Hamisa alisema tu kwamba, “Nimekuza” kwenye picha hiyo, lakini kilichofuatia kwenye upande wa kutoa maoni ni kama Hamisa aliongeza kuni kwenye moto uliokuwa umeanza kufifia kuhusiana na suala zima la Diamond kujitenga mbali na mtoto huyo.

Inaaminika kwamba Diamond ndiye baba mzazi wa Dylan, lakini vitendo vyake baridi kuelekea kwa mtoto huyo katika miaka ya hivi karibuni vimekuwa vikiibua maswali, baadhi wakiitisha uthibitisho wa DNA.

Lakini safari hii, wengi walisema kwamba picha mpya ya mtoto huyo inaonyesha chembechembe za Diamond kwa mbali na kusema kwamba msanii huyo wa WCB Wasafi atakuja kuumbuka ukweli ukidhihirika.

“Mbona kama namuona Diamond mtupu tena 😢😂😂😂🙌 Mungu mkali nyie,” Diana Rosey.

“MUNGU anajua kuumbua watu weee twende tu majibu yanakaribia kupatikana hata bila DNA 🤣🤣🤣🙌” Lucy Bedsheet Solution.

“Yaani kafanana na mama Diamond, Mungu wa ajabu nyie.” Irene Fabian.

“Weeee MashaAllah amechange sikujua kama ni yy ka handsome huyu atakuwa president wa tz mpaka mtashangaa” Mimalitho.