Hakuna mkate mgumu mbele ya chai: Stevo Simple Boy afanikiwa kumpata Betty Kyallo

Baada ya kumfukuzia kwa muda, hatimaye msanii Stevo Simple Boy amefanikiwa kumpata kichuna wa ndoto zake, mwanahabari Betty Kyallo.

Muhtasari

• Kwa kipindi cha kama wiki tatu hivi, msanii huyo wa Freshi Barida amekuwa akimfukuzia Kyallo ambaye kipindi chote hicho alitia masikio yake nta.

Stevo Simple Boy ampeleka Betty Kyallo date
Stevo Simple Boy ampeleka Betty Kyallo date
Image: Instagram

Baada ya kumfukuzia kwa muda, hatimaye msanii Stevo Simple Boy amefanikiwa kumpata kichuna wa ndoto zake, mwanahabari Betty Kyallo.

Kupitia Instagram, Stevo Simple Boy alipakia msururu wa picha baada ya kukutana na Stevo na kuelekea katika mgahawa wa kifahari kwa ajili ya chakula cha alasiri.

Msanii huyo baada ya kumtia Kyallo viganjani mwake – na kutimiza ndoto yake ya muda mrefu – alisema kwamba moyo wake umetulia sasa.

Stevo alidokeza kwamba katika kikao hicho, hakuwa mzembe bali aliumwaga moyo wake wazi wazi kwa Kyallo kuhusu jinsi anavyompenda na kumtaka amrudishie jibu hivi karibuni kama walivyoagana.

Kwa kweli Roho Yangu Sasa Iko welo welo.. nilipeleka crush wangu date .. Mungu ni mwema nakupenda sana Betty kyalo.... fikiria hio Mambo yangu tumeongea leo.nasubiria jibu!” Stevo Simple Boy alisema.

Kwa kipindi cha kama wiki tatu hivi, msanii huyo wa Freshi Barida amekuwa akimfukuzia Kyallo ambaye kipindi chote hicho alitia masikio yake nta.

Hivi majuzi, Stevo kupitia Instagram alipakia picha ya Kyallo na kufichua kwamba katika mwili wake, anawaona wanawe watatu, wavulana wawili na msichana mmoja na kumtaka Kyallo kufanya hima kabla mayai hayajaviza.

“Me nikipata Betty kyalo na settle tu..na anizalie watoto watatu boys wawili na Dem mmoja .God bless 🙏🏼🥰 Mungu hii yotee uliumba wewe mwenyewe 😊. naomba Sasa unibariki nayo,” Stevo alitupa ndoana.

Ama kweli hakuna lisilowezekana chini ya jua pakiwepo nia.