Zuchu ameomba radhi kwa kuimba matusi wakiwa na Diamond Zanzibar

Awali tuliripoti kwamba msanii huyo alikuwa ameimba akitema cheche kwa wanaotaka yeye kuachana na Diamond kwamba jambo hilo haliwezekani hata "mmpe mkun**".

Muhtasari

• Sasa ni kutokana na tusi hilo ambalo msanii huyo amelazimika kuomba radhi baada ya kufika katika ofisi za BASATA na kukabidhiwa muongozo wa kanuni na sheria zake.

Zuchu
Zuchu
Image: Facebook

Zuhura Othmn Soud maarufu kama Zuchu, msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi hatimaye ameomba radhi kwa mashabiki wake lakini pia kwa chama cha kusimamia maadili ya Sanaa Tanzania, BASATA kutokana na matamshi ya matusi aliyoyatoa kwenye wimbo akiwa na Diamond wiki jana visiwani Zanzibar.

Awali tuliripoti kwamba msanii huyo baada ya kuandika kwamba ameachana na Diamond, alionekana naye katika shoo ya Full Moon Party kisiwani Zanzibar na akiwa jukwaani aliwatolea pofu watu, haswa kina dada ambao wanaomba aachane na Diamond.

Akiimba, Zuchu alisikika akitamka;

“Ila wacha tutume taarifa kwa upande wa pili si ndio? Wanaohisi watamchukua [Diamond], nawaona mnamaliza Miungu, mnamaliza mikao na utundu, huyu kwangu hapa hatoki hata mmpe mkun**…”

Sasa ni kutokana na tusi hilo ambalo msanii huyo amelazimika kuomba radhi baada ya kufika katika ofisi za BASATA na kukabidhiwa muongozo wa kanuni na sheria zake.

Katika barua iliyoonekana na radiojambo.co.ke, Zuchu aliandika;

“Kwa wapendwa wetu wa Sanaa, Napenda kutumia fursa hii kuwaomba radhi kutokana na maneno niliyoyatumia kwenye kibwagizo ambacho kilileta taharuki kwenye tamasha la Full Moon party – Kendwa Beach Zanzibar hivi karibuni.”

“Najua kuwa maneno yameleta sintofahamu kwa wengi wenu na kuleta maana hasi kwa jamii na mashabiki zangu kiujumla.”

“Nia yangu ilikuwa kuleta burudani njema na furaha kwa mashabiki wangu wote. Si lengo langu kupotosha, kumomonyoa maadili na kuleta taharuki kwa yeyote.”

“Ninachukua ahadi leo kufanya kazi na timu yangu ili kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena kwenye matamasha yajayo.”

“Nawaomba radhi tena kwa jamii na baraza la Sanaa (BASATA) ambao ndio walezi wangu.”