Embarambamba adai kupigiwa simu ya 'private' akitishiwa maisha pamoja na familia yake

Msanii huyo alisema kwamba hajawahi kosea mtu na muda wote anajishughulisha na maisha yake ya kutafutia familia riziki kwa sarakasi zak za injili za kujivuruga kwa matope na kuparamia miti.

Muhtasari

•"Halafu kitu kingine mimi nahitaji maombi kwa kuwa kuna kitu kingine unaweza ukasikia kama mchezo mchezo kwa vyombo vya habari, upate kimetokea kuwa kibaya." alisema.

Embarambamba
Embarambamba
Image: Facebook

Msanii wa injili kutoka Kisii, Chris Embarambamba ameibuka na madai mapya akidai kwamba amekuwa akipigiwa simu fiche na mtu ambaye hamjui akimtishia maisha yake pamoja na familia yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Embarambamba aliapakia video akitoa malalamishi hayo kwamba kuna mtu ambaye amempigia simu na namba fiche huku akimtishia maisha yake.

Msanii huyo aliwaomba mashabiki wake kumweka kwenye maombi kwani mambo mengine yanaweza yakaanza kama mzaha lakini yakaishia kwa tukio baya.

“Mashabiki, nawaomba kwa kunyenyekea sana, kama hunipendi, wacha kunipigia simu ya private, ukinitishia maisha yangu pamoja na ya familia yangu, watoto wangu. Mimi hii kazi nafanya ya injili ni kujivuruga ndani ya matope na kulala. Lakini maneno ya kunitishia maisha na familia yangu, tafadhali naomba niacheni peke yangu na maisha yangu,” Embarambamba alisema.

Msanii huyo alisema kwamba hajawahi kosea mtu na muda wote anajishughulisha na maisha yake ya kutafutia familia riziki kwa sarakasi zak za injili  za kujivuruga kwa matope na kuparamia miti.

“Kwa sababu hii matope najivuruga ndani, kupanda miti, mimi sijakuja kukosea mtu. Halafu kitu kingine mimi nahitaji maombi kwa kuwa kuna kitu kingine unaweza ukasikia kama mchezo mchezo kwa vyombo vya habari, upate kimetokea kuwa kibaya. Tafadhali nawaomba mjniombee lakini maneno ya kunitishia maisha tafadhali niacheni kabisan,” alimaliza.

Kuhusu suala la kesi yake na KFCB, Embarambamba alisema kwamba hivi karibuni atapokea majibu kutoka kwa bodi hiyo ya Sanaa akisema kwamba mawakili wake Danstan Omari na mbunge Silvanus Osoro wanaendelea kujifanyia kazi.