Diamond mwenyewe ndiye anajua ukweli kuhusu mtoto wa Hamisa, hata mimi sijui - Zari

“[Diamond] akiniambia huyu ni mtoto wangu nataka ajuane na hawa nitamkaribisha, lakini kwa sasa hakuna mawasiliano rasmi kwa hiyo sijui kuhusu hilo,” Zari aliongeza.

Muhtasari

• Zari alisimama kwenye njia kuu na kusema kwamba Diamond pekee ndiye anayejua ukweli wote kama mtoto ni wake au la.

Zari
Zari
Image: Screengrab

Zari Hassan ambaye ni mzazi mwenza na Diamond Platnumz amezungumzia suala la utata unaomzunguka mtoto wa Hamisa Mobetto.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa chapa ya Softcare nchini Tanzania, Zari alisema kwamba utata unaozunguka mtoto Dylan kuhusu ikiwa Diamond ni babake kweli au ni kuzingiziwa hata yeye hajui.

Zari alisimama kwenye njia kuu na kusema kwamba Diamond pekee ndiye anayejua ukweli wote kama mtoto ni wake au la.

“Yaani hapo kabisa ndio sijui, Diamond mwenyewe ndio atajielezea kama yule mtoto ni wake, kama sio wake, kwa hiyo Zaidi na hapo mimi sijui kabisa,” alisema kwa msisitizo.

Aidha, mama huyo wa watoto watano, wawili wakiwa wa Diamond alifichua kwamba yeye hana shida yoyote kuhusu mtoto wa Hamisa kujumuika na wanawe, mradi tu Diaomond amwambie kuwa ni mwanawe.

“[Diamond] akiniambia huyu ni mtoto wangu nataka ajuane na hawa nitamkaribisha, lakini kwa sasa hakuna mawasiliano rasmi kwa hiyo sijui kuhusu hilo,” Zari aliongeza.

Itakumbukwa maswali mengi yaliibuliwa mwaka jana baada ya Diamond kutembea na wanawe kutoka kwa Zari na Tanasha Donna kwenye ndege pasi na uwepo wa mwanawe kutoka kwa Hamisa Mobetto.

Kwa muda sasa, Dylan amekuwa akikumbwa na maisha yenye utata mwingi mitandaoni, baadhi wakihisi mtoto huyo si wa Diamond na wengine wakisimama upande wa kuwa mtoto ni wa Diamond.

Hata hivyo, si Diamond wala Hamisa ambaye amewahi jitokeza hadharani na kukanusha au kukiri kuhusu madai hayo, suala lote likiachiwa wadadisi na majasusi wa mitandaoni.