Hatimaye Mulamwah anunua gari, "Kijana wa Kitale sasa ni former pedestrian!"

Mulamwah kununua gari kunakuja wiki chache baada ya kuhamia nyumba mpya kutoka kwa ile aliyokuwa akiishi zamani.

Muhtasari

• Mchekeshaji huyo aliwashukuru mashabiki wake kwa kumuombea muda wot mpaka ametimiza ndoto ambayo wengi wamekuwa wakimdhihaki kwamba asigneifanikisha.

MULAMWAH
MULAMWAH
Image: FACEBOOK

Baada ya kusemwa sana kuwa ni mtu maarufu asiye na gari, mchekeshaji Mulamwah ambaye pia anajiongeza kama mtangazaji wa redio amenunua gari.

Mulamwah kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mulamwah alipakia picha akiwa mbele ya gari aina ya Mercedes jeusi na kusema kuwa ni mmiliki mpya mjini wa gari hilo la kifahari.

Mchekeshaji huyo aliwashukuru mashabiki wake kwa kumuombea muda wot mpaka ametimiza ndoto ambayo wengi wamekuwa wakimdhihaki kwamba asigneifanikisha.

“MUNGU ALIFANYA 💪🙏 mmiliki wa gari la fahari 💯 mercedes BENZ E250. Kila mara tembea polepole lakini sogea ipasavyo, inanipasa kumshukuru Mungu kwa baraka zote maishani. Wacha tuanzie maisha hapa. Asante kwa familia, mashabiki na marafiki kwa usaidizi wenu na maombi kila wakati,” Mulamwah alisema.

Baba huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba sasa angalau mkewe Ruth K atakuwa anamwahisha mtoto kliniki kwa muda wakiwa ndani ya gari.

“Kijana wa kitale sasa ni former pedestrian. Kalamwah na mama Kalamaz sasa watakuwa wanafika kliniki kimtindo. @atruthk asante kwa support daima mamake,” alisema.

Mulamwah kununua gari kunakuja wiki chache baada ya kuhamia nyumba mpya kutoka kwa ile aliyokuwa akiishi zamani.

Mulamwah kwa muda amekuwa akiishi nyumba yenye chumba kimoja cha kulala kwa muda licha ya kutoboa maisha mjini muda mrefu, jambo ambalo alijitetea akisema kwamba ndoto yake kuu ilikuwa kujenga jumba la kifahari kijijini kwao Kitale.

Baada ya kukaribia kumaliza ujenzi wa jumba hilo, Mulamwah alihamia nyumba nzuri na kusema kwamba ni wakati wa kuserereka kimaisha sasa, kwani nyumba yake kijijini sasa imekaribia kufika tamati katika ujenzi.